Hebu basi tupe misingi ya kisheria basi...Kwa nini unadhani kesi inaweza kutupwa na DPP (Nolle presequi)?
Mbona aliodoka sehemu ya tukio, halafu akarudi tena? Hii haiwezi kujenga mazingira kwamba alienda pembeni akakaa na kupanga kitu cha kufanya?
Hapa itabidi niwatafute maloya (lawyers) wanipe mwanga kidogo!!
Babu DC
tuongee ukweli, heat of passion hapo bado ilikuwa haijaisha. huwezi jua ni kwanini aliondoka na kurudi pale stand, labda kuna kitu cha muhimu alikuwa ameenda kukifanya pale au alikuwa anakifanya pale, hivyo alivyoondoka, alifikiri labda mwanamke yule atakuwa ameshaondoka. kutembea na mwanaume mwingine hiyo haikumuumiza sana....ila kitendo cha mwanamke kumtukana mwanaume stand kwamba hana nguvu za kiume, na kwamba hata watoto wale si wake ni wa mwanaume mwingine aliyemsaidia, maneno hayo ni wazi kwamba hayakuondoka mapema kichwani mwa mwanaume yule, nafikiri yalikaa katikati ya ubongo wake hata zaidi ya wiki au miezi. sasa kitendo cha yeye kuondoka, naweza sema kuwa alitaka kuepusha shari kama alivyokuwa amezoea kuepusha shari kipindi cha nyuma alipokuwa akiletewa mwanaume na kufuatwafutwa hata bar na mwanaume na mkewe. nafikiri alikuwa anaondoka pale stand alipokuwa amevuliwa nguo kuepusha shari.
alipofika mbali, aliamua kudrive kurudi, labda kuja kumzuia yule mwanamke asiendelee kumchafua pale stand, kwasababu huwezi jua, alipoondoka yeye aliendelea kurap yoyoo you know what i am saying.... pale stand kumwanika ex wake. ningesema mwanaume alirudi pia ili kumwondoa mwanamke pale kwa amani ili wakayaongee nyumbani, lakini ghafla, ALIPOMWITA NA KUMWONA YULE MWANAMKE ANAKUJA, GHAFLA KICHWANI MWAKE ALIYAKUMBUKA YALE MATUSI, HANA NGUVU ZA KIUME, WATOTO ALISAIDIWA, AMEANIKWA HIVYO STAND, hasira kubwa sana ikamjia kichwani kwake, akajikuta ameamua kumshambulia kwa kumgonga na gari.
jambo hilo hatuwezi kusema ya kuwa alilipanga kabla. wasnt pre-meditated kabisa. pia, maneno hayo ni makali sana, katika jamii yeyote ile yanaweza kuamsha hasira kali kufanya tukio lisilo la kawaida. pia, heat of passion ilitulia alipoondoka, lakini aliporudi na kuwita mwanamke aje kwenye gari, alipomwona, kukumbuka tu yale maneno hasira ilimjia tena ghafla akafanya alichokifanya.
hata jaji mwenyewe atakayesikiliza kesi hii, akifanyiwa kitendo kama hicho, atafanya jambo kubwa kuliko hili alilofanya uyo mwanaume. any ordinary person katika jamii akikutana na jambo hili, atafanya kitu kikubwa.
historia inayonesha kuwa, huyu jamaa alikuwa na uvumulivu sana, alishavumilia sana kuletewa wanaume na huyu mwanamke, siku zote alivumilia, lakini jambo alilokutana nalo mwishoni pale stand lilikuwa juu ya uwezo wake. what do you think would be a reasonable time for the heat of passion to cook kwa maneno kama yale? hata kama principle ni kwamba alitakiwa awe amefanya tukio kubwa wakati uleule wa maneno makali kabla hajaondoka, lakini kwa any ordinary person hakika kichwa chake kilikuwa hakijatulia kwa muda mrefu kuliko....
NB; nimejitahidi kuongea kama layman, lakini kusema ukweli, ni nusu kwa nusu, si rahisi sana kutumia defence hii ya provocation, pamoja na kwamba inawezekana, na labda yeye ataanzisha principle mpya kupitia kesi yake (kulingana na kesi nyingi zilizopita, heat of passion hapa ilikuwa imeshatulia pale alipoondoka) lakini kila kesi huamuliwa kulingana na facts zake. kitendo chake cha uvumilivu kabla, na ukali wa maneno yale (pengine aliwapenda sana wale watoto, walikuwa moyoni mwake, pengine pia aliamua kuoa mwanamke mwingine ambaye alikuwa hajazaa na hivyo angesikia kuwa hana nguvu basi tena, pengine kuna watu wengi wanamfahamu pale na yeye alianikwa kuwa hana nguvu na watoto alisaidia...hakika hapa anastahili provocation kama mimi ningekuwa jaji)....ciao.