Nasra: Wazanzibari kudai haki yao sio ubaguzi

Nasra: Wazanzibari kudai haki yao sio ubaguzi

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mwakilishi wa Viti Maalum kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Dkt. Nasra Nassor amesema kuna haja ya vijana wa Zanzibar na Tanganyika kujua haki zao katika masuala ya Muungano.

Dkt. Nasra alizungumza hayo Juni 15, 2026, wakati akichangia makadirio ya Bajeti Kuu ya Serikali ya Zanzibar ndani ya Baraza la Wawakilishi, ambapo aligusia haki na nafasi ya vijana wa pande zote mbili za Muungano.

Dkt. Nasra amesisitiza kuwa ipo haja ya kuwa na muundo mzuri na unaoeleweka wa Muungano ili vijana watambue nafasi zao katika masuala ya haki na usawa, huku akifafanua kuwa Wazanzibari kudai haki zao isihesabiwe kama ubaguzi.

“Tunaambiwa kwamba labda Wazanzibari wakizungumza suala la Uzanzibari linaonekana ni suala la kibaguzi, lakini si suala la kibaguzi kwa sababu Watanganyika wana nafasi yao katika Muungano na Wazanzibari wana nafasi yao. Ni kwa sababu tu ya 'foundation' (msingi) ya Muungano imekosekana ndio maana tunaona labda ajira hizi ni za kwao na hizi sio za kwao. Tuseme tu Tanganyika yenyewe inahitaji muundo unaoeleweka,” amesema Dkt. Nasra.

 
Mbona wabara ndio tunaongoza kwa kuwabagua Wa Zanzibar mada nyingi kwenye mitandao ya kijamii ni za kukataa muungano na kuwabeza Wa Zanzibar nchi yetu sote hii.
 
“Tunataka kuona katika Taifa hili vijana jeuri na wenye kujiamini , si vijana waoga ,akina ndiyo bwana mkubwa, vijana wenye ujasiri wa kuhoji na kupiga Vita mfumo wa jamii isiyo shabihiana na matakwa na matalajio ya jamii ya Kitanzania. Tunataka vijana waasi dhidi ya mfumo kandamizi, ubwana na ufisadi katika Taifa”.

Mwalimu JK Nyerere.
 
Back
Top Bottom