Nasubiria kwa hamu vita ya Ukraine iishe nikatafute kazi

Nasubiria kwa hamu vita ya Ukraine iishe nikatafute kazi

Kool the gang

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
497
Reaction score
1,465
Binafsi sijui vita vya Ukraine itaisha lini, lakini naimani Kwamba Ile vita siku ikiisha tu, kutakuwa na ujenzi mkubwa sana wa miundombinu chini ya ufadhili wa nchi washirika wa Ukraine, ambao ni USA na mataifa ya EU, hivyo manpower kubwa sana itahijika na kazi zitakuwa nyingi sana za ujenzi. Bufa, The Icebreaker, Lusungo, Dr Matola PhD, britanicca Myahudi Jr II , Isanga family, Kim Jong Jr, Maghayo, Chaliifrancisco DR HAYA LAND, Jebel, Forgotten, Black Sniper, Masanja,Jimena, mwandende Richard mnaoje haya mawazo yangu wakuu?.
 
Cha muhimu serekali iongee na yukreni, kuwa watanzania wapo tayari kuja kufanya kazi ya kuijenga yukreni mpya.

Hivyo serekali ya yukren ikihitaji man power ni simu moja tu Tanzania
 
Binafsi sijui vita vya Ukraine itaisha lini, lakini naimani Kwamba Ile vita siku ikiisha tu, kutakuwa na ujenzi mkubwa sana wa miundombinu chini ya ufadhili wa nchi washirika wa Ukraine, ambao ni USA na mataifa ya EU, hivyo manpower kubwa sana itahijika na kazi zitakuwa nyingi sana za ujenzi. Bufa, The Icebreaker, Lusungo, Dr Matola PhD, Myahudi Jr II Jr II, Isanga family, Kim Jong Jr, Maghayo, Chaliifrancisco fransisco, DR HAYA LAND, Jebel, Forgotten, Black Sniper mnaoje haya mawazo yangu wakuu?.

Kama unataka fursa hiyo basi wakati muafaka kabisa wa kwenda huko ni sasa wakati Vita ikiwa bado inaendelea.

Vita ikiisha Watu wenye nafasi nzuri zaidi ya kupata fursa za Ajira au kazi huko Ukraine ni wale Watu ambao wamekuwa wakiwasaisia raia wa nchi hiyo katika nyakati ngumu za VIta
 
Cha muhimu serekali iongee na yukreni, kuwa watanzania wapo tayari kuja kufanya kazi ya kuijenga yukreni mpya.

Hivyo serekali ya yukren ikihitaji man power ni simu moja tu Tanzania
Kwa Serikali hii mkuu futa wazo, kwasasa wao wanawaza uchaguzi tu.
 
Binafsi sijui vita vya Ukraine itaisha lini, lakini naimani Kwamba Ile vita siku ikiisha tu, kutakuwa na ujenzi mkubwa sana wa miundombinu chini ya ufadhili wa nchi washirika wa Ukraine, ambao ni USA na mataifa ya EU, hivyo manpower kubwa sana itahijika na kazi zitakuwa nyingi sana za ujenzi. Bufa, The Icebreaker, Lusungo, Dr Matola PhD, Myahudi Jr II Jr II, Isanga family, Kim Jong Jr, Maghayo, Chaliifrancisco DR HAYA LAND, Jebel, Forgotten, Black Sniper, Masanja mnaoje haya mawazo yangu wakuu?.
Twende mkuu, mwezi ujao nitasogelea karibu kabisa nchi ya Poland
 
Ngoja tuwasubirie wazee wa majuu, hao niliowatagi binafsi passport ninayo na nauri ninayo labda waninyime viza tu mkuu.
Kama passport na nauli unayo tafuta sasa visa ya Poland au Romania hapo ni jirani kabisa na ukraine
 
Cha muhimu serekali iongee na yukreni, kuwa watanzania wapo tayari kuja kufanya kazi ya kuijenga yukreni mpya.

Hivyo serekali ya yukren ikihitaji man power ni simu moja tu Tanzania
Tanzania haiku unga mkono hadharani au moja kwa moja, vita vya Ukraine na Russia hivyo usitegemee 'share' wakati wa ujenzi. Unakumbuka mzozo wa Kidiplomasia ulio zuka wakati Dr Tulia Ackson alipoenda Moscow aka kutana na President Putin? Kiyv ilitaka Dr Tulia kukutana na Zelensky kwanza kabla ya kwenda Moscow. The rest is history.
 
Dah! Mkuu Urusi bado anashua mabomu yake ujue.
Ndiyo, Vita bado inaendelea. Huu Ndio muda mzuri zaidi wa Watu Wahamiaji kuweza kwenda huko Ukraine. Kwa Sasa hivi kwenda nchini Ukraine hakuna vikwazo vyovyote vile vya kuomba Viza, hata nauli ya kwenda huko unaweza kupatiwa kutoka kwa Serikali ya huko au kutoka kwa tawala zingine za nchi za Magharibi ambazo ni marafiki wa Utawala wa Ukraine.

But all in all, milango yote kabisa ya kupatiwa uraia wa nchi hiyo ya Ukraine ipo wazi kabisa kwa Watu wote wenye nia ya dhati ya kwenda huko Ukraine kwa wakati huu. Kuna Watu kadhaa nianaowafahamu tayari wameshaingia kwenye scheme ya namna hii, Walienda huko kama Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Vita ilipoibuka wao hawakutaka kurejea kwenye nchi zao walikotokea na badala yake walijiunga na Vikosi vya Wapiganaji wa Ukraine na sasa tayari wamepewa Haki za uraia wa nchi hiyo, now they've the Dual citizenships.
 
Vita haziwezi kuisha maana Kuna uasi utaanza WA ndani Kwa ndani Kwa slwasiokubaliana na sera za zelensky.

Iraq,Libya, Afghanistan n.k

vita zao dhidi ya mabeberu iliisha Ila Bado wananyukana wao Kwa wao Hadi leo hii.

Kwaiyo Ni RISK bado
 
Kwa Ukraine hali kidogo ipo tofaufi Sana na hizo nchi ulizotaja. Ni kweli Watu wa Ukraine Wana tofaufi zao za kisiasa, lakini tofaufi zao hizo haziwafanyi wao kwa wao kufarakanishwa kabisa na kuanza kupigana Vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kwa kiasi kikubwa Sana Utawala uliopo huko Ukraine unaungwa mkono na Wananchi wengi zaidi wa nchi hiyo. Watu wa Ukraine wameungana Sana ukilinganisha na jinsi hali ilivyo nchini Urusi.
Raia wengi zaidi wa Ukraine hawataki tena kuwa chini ya Utawala wa Kidikteta wa Urusi, wengi sana bado wanaendelea kukumbuka dhahama na madhila waliyopata kutoka kwa Wanajeshi katili Sana wa iliyokuwa Idara ya Ujasusi ya KGB ya Serikali ya Urusi ya zamani (USSR). KGB waliwafanyia USHETANI mbaya sana Raia wa nchi hiyo ya Urusi, hali iliyowalazimisha Wananchi wengi Sana wa nchi hiyo ya Urusi (USSR) kuanzisha harakati za UASI wa chini chini dhidi ya KGB na Serikali ya Urusi.

Kumbuka: Huyu Rais Vladimir Putin wa Urusi hii ya sasa aliwahi kuwa Mkuu wa Idara ya Ujasusi ya KGB, Watu wa Ukraine wanamfahamu vizuri Sana. Raia wa Ukraine kamwe hawawezi tena kukubali kurudi tena utumwani Misri!
 
Binafsi sijui vita vya Ukraine itaisha lini, lakini naimani Kwamba Ile vita siku ikiisha tu, kutakuwa na ujenzi mkubwa sana wa miundombinu chini ya ufadhili wa nchi washirika wa Ukraine, ambao ni USA na mataifa ya EU, hivyo manpower kubwa sana itahijika na kazi zitakuwa nyingi sana za ujenzi. Bufa, The Icebreaker, Lusungo, Dr Matola PhD, britanicca Myahudi Jr II , Isanga family, Kim Jong Jr, Maghayo, Chaliifrancisco DR HAYA LAND, Jebel, Forgotten, Black Sniper, Masanja,Jimena, mwandende Richard mnaoje haya mawazo yangu wakuu?.
Ukiona kweli wamesitisha vita unakaa kidogo ili usije ukaenda ukakwama maana Trump haeleweki ila huko kazi zipo hasa Ukraine na wana Technology nzuri wale jamaa unaweza ukaokota kitu..usisubiri eti Serikali itatangaza hakuna kitu kama hicho..
 
Kazi hata sasa zipo na sio lazima Ukraine tu. Ukisubiri fursa utasubiri sana.
 
Back
Top Bottom