Wakuu mko poa?
moja kwa moja kwenye mada
Sasa hivi nakuwaga na Safari kibao za kwenda Mbezi stendi ya mabasi ya mikoani
Sasa kila mara nakutana na changamoto ya hawa watafuta riziki pale Mbezi stand
Changamoto yenyewe ni kwamba nakereka na watu ambao wakikuona tu wanaanza kukuuliza bosi vipi unaenda ofisini?
Unakwepa huyu unakutana na mwingine bosi vipi unaenda ofisini? Mimi najibu hapana naenda kupokea watu
Sasa juzi nikajisahau mmoja mwana dada alivyoniuliza bosi unaenda ofisini nikajibu ndio tukaongozana tunafika sehemu niliozoea kuingilia ambayo wengi ndio wanapita akaniambia bosi ofisini sio huko ni huku ananionesha tupande kule juu, Mimi nikamwambia dada naenda kupokea wageni.
Nikamwambia samahani kwa usumbufu nikamtoa buku tano nikaingia zangu ndani kusubiri wageni
Sasa wakuu wazoefu naomba mnijuze kule juu wanakoita ofisini watu wanaendaga kufata nini?
Nitoeni ushamba wakuu.