Nasumbuliwa na kikohozi kikavu

Abie

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
289
Reaction score
535
Wanabodi, salaam! Ni mwaka sasa hili tatizo linanisumbua ( kikohozi kikavu) nimeenda hospitali mpaka nimechoka, nimekunywa dawa za hospitali na kienyeji mpaka nimechoka; kikohozi hakiponi.

Napata shida sana na kwasasa naona mpaka kifua kinauma sana mwanzo kilikuwa hakiumi nilikuwa nakohoa tu na huku kukohoa ni kwa namna ya clearing the throat yaan sikohoi mpaka nikatoa makohozi. Sasa saaa hivi nakohoa hicho kikohozi kikavu na kifua kinauma.

Nashangaa sana kikohozi gani kisichopona hata sasa natumia syrup ya good morning lkn wapi hakiponi, natafuna tangawizi bado nimetumia asali, karafuu na dawa zingine lkn bado.

Kwahiyo wadau najua JamiiForums ni nyumbani kwa wataalam wa kila aina naombeni msaada wenu niweze kuondokana na hali hii.
 
Asante kwa ushauri, huo mchanganyiko niliwahi kutengeneza haikufaa kitu, na kuhusu minyoo nilienda kupima nikakutwa nayo nikatumia dawa lkn ndo hivyo tena hali bado tete ndugu
 
Tumia mimea yenye sulphur ya asili. Pia kama upo maeneo yenye maji ya chemchem yatakubariki sana kaka.
 
Hiyo ni COVID 19. Tafuta ampiclox, fanya mazoezi, tangawizi
 
Asante kwa ushauri, huo mchanganyiko niliwahi kutengeneza haikufaa kitu, na kuhusu minyoo nilienda kupima nikakutwa nayo nikatumia dawa lkn ndo hivyo tena hali bado tete ndugu
Ulitumia dawa gani ya minyoo??
 
Sikutishi ila kikohoo cha mda mrefu kinaweza kuwa kansa ya mapafu God forbid [emoji724]

Lung cancer huanza hivyo kwa kikohoo cha mda mrefu
Muulize Dr mkuu na ukapime pia
 
Sikutishi ila kikohoo cha mda mrefu kinaweza kuwa kansa ya mapafu God forbid [emoji724]

Lung cancer huanza hivyo kwa kikohoo cha mda mrefu
Muulize Dr mkuu na ukapime pia
Vipi kihusu kikohozi cha upande mmoja wa koo kuwasha ? Pakiwasha nakohoa ila sio sana, Hosp walinipa dawa sikupona niliporudi nikashauriwa nisilalie ubavu Wa kulia kikapona kama miezi misili
Sasq kimerudi tena,kwa asubuhi nakohoa sio zaidi ya mara kumi
 
kamuone mtaalamu wa ENT karibu yako
 
Maybe ni :-
1.Asthma- mara nyingi wanakuwa na allergy flani , kwenye familia au ukoo kunakuwa na mtu mwenye allergy, na wanakohoa mara nyingi asubuhi au jioni

2. Post nasal drip syndrome: hawa wanakuwa na kama makohozi yanachuruzika kutoka nyuma kama ya pua kwenda kooni na huwa yananuka

3: laryngopharyngo reflux : hawa wanakuwaga na acid inapanda kutoka tumboni kuja kooni , anakuwa anaiskia ina radha ya uchachu, koo linakauka mara kwa mara , anameza mate mara kwa mara, anaskia kama kuna kitu kooni, anakuwa anakohoa kidogokidogo ili kuondoa tuvitu flani kooni, na mara nyingi kikohozj kinakuwa kikavu na hutokea baada ya kushiba na kwenda kulala

4:rhinosinusitis: kamasi, masikio kutosikia vizuri, kichwa kuuma mbele

5.TB: kwa mwaka mzima bila dawa ingekuwa ni mbaya yaani ungekuwa ushakonda sana na mara nyingi unakuwa na dalili nyingine kama kutokwa jasho usiku na homa , kuvimba tezi,

6.cancer: kwa mwaka bila dawa ungekuwa na hali mbaya zaidi yaani ungekuwa una kohoa na damu, kupungua uzito , kupumua kwa shida na ingekuwa imesambaa sehemu nyingine

7: moyo: unakuwa mara nyingi unapata shida ya kupumua ukilala flat, unasikia moyo unadunda sana, unavimba miguu,

8: dawa : kuna dawa ACEI kama captoril wanatumia watu wa moyo huwa zinaleta kikohozi

9: sarcoidosis
10: COPD

NOTE: ziko nyingi sana ila 5 za mwanzo ndo zinawakuta wengi cha msingi historia yako haijitoshelezi kujua tatizo ni lipi kati ya hayo hapo juu na bado hapo hujafanya kipimo chochote

Hivyo kumwona daktari tena wa magonjwa ya upumuaji au kifua (pulmonologist) na ENT pia ni lazima na haraka kwa sababu magonjwa 5 hapo chini ni hatari sana kama ndio chanzo hivyo yanahitaji kubainiwa mapema na kutibiwa haraka iwezekanavyo kabla hayajafikia hatua mbaya zaidi ingawa kwa jinsi ulivyoeleza ni kama 5 ya juu ndo tatizo ambayo hayatishi sana.
 
Kwa kweli Sina uhakika na hilo ila hili la kukohoa sana huwa wanaweka matangazo hata hospital za huku na kwenye vipindi pia [emoji636]

Ungeenda hospital nzuri wakakupima kwa vipimo kama una mashaka

Huu uzi ni wa zamani ndio nimeuona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…