Abie
JF-Expert Member
- Jul 15, 2021
- 289
- 535
Wanabodi, salaam! Ni mwaka sasa hili tatizo linanisumbua ( kikohozi kikavu) nimeenda hospitali mpaka nimechoka, nimekunywa dawa za hospitali na kienyeji mpaka nimechoka; kikohozi hakiponi.
Napata shida sana na kwasasa naona mpaka kifua kinauma sana mwanzo kilikuwa hakiumi nilikuwa nakohoa tu na huku kukohoa ni kwa namna ya clearing the throat yaan sikohoi mpaka nikatoa makohozi. Sasa saaa hivi nakohoa hicho kikohozi kikavu na kifua kinauma.
Nashangaa sana kikohozi gani kisichopona hata sasa natumia syrup ya good morning lkn wapi hakiponi, natafuna tangawizi bado nimetumia asali, karafuu na dawa zingine lkn bado.
Kwahiyo wadau najua JamiiForums ni nyumbani kwa wataalam wa kila aina naombeni msaada wenu niweze kuondokana na hali hii.