Mkuu, kabla ya kuishi na huyu mwanamke uliye naye sasa.....ulishawahi kumdanganya mwanamke yeyote kuwa utamuoa? Matatizo mengine ni sisi wanaume wenyewe tunajitakia, mtu anakuwa na nyege anahamua tu kumdanganya mwanamke ili apewe show mara baada ya hapo anaingia mitini. Unampa matumaii mtoto wa watu unategemea nini? Sikulaumu ila makala yako yamenikumbusha tukio lililomtokea mjomba wangu miaka ya nyumba (in the 90s). Alikuwa anamla mtoto wa watu baada ya kumdanganya kuwa atamuoa na akawa anamtambulisha kwa baadhi ya marafiki zake, mwisho wa siku akamtema. Demu akapoteza dira akageukia kwa babu na kumkomoa mjomba wangu. Mjomba alikuja kuugua sana na kukondeana mpaka watu wakahisi ana ukimwi. Mke aliyekuwa anatembea naye baada ya yule aliyemdanganya kuoa akaja kufa katika mazingira ya kutatanisha. Alikufa porini kule Temeke kwa Limboka, yaani aliondoka nyumbani akiwa anapika. Mjomba anarudi anakuta chakula kiko jikoni mke hayupo na kila kitu ndani kiko fresh. Mjomba akakaa mpaka usiku kusubiri mke arudi lakini wapiiiiiii, Asubuhi yake mjomba akaenda kutoa ripoti polisi, mke akaja kupatikana siku ya tatu porini kajiua kwa kujificha. Baada ya hapo, mjomba alikuja kupata maradhi ya hajabu, mara uume usinyae na pumbu kujaa maji au pumbu moja kuwa kubwa kama mshipa (puto) ila akipimwa hospitali hana ugonjwa wowote. Mjomba kapona majuzi tu 2015 baada ya kupata mateso kwa miaka yote hiyo. Kazeeka na hana mtoto wala kuwa na hamu ya mwanamke. Pole mkuu sikutishii hapa ila nakupa ushuhuda tu.