Natabiri Elon Musk wa Tesla/Twitter kumpiga KO Mark Zuckerberg wa Facebook kwenye Pambalo lao la Masumbwi

Natabiri Elon Musk wa Tesla/Twitter kumpiga KO Mark Zuckerberg wa Facebook kwenye Pambalo lao la Masumbwi

Labda amuelemee kwa uzito. Ila Mark ni mtaalam wa stadi za Mapigano ikiwemo Kung Fu nk.

Ila kwa sababu Elon ana umbo kubwa lisababishwalo na kula Donati kila siku, anaweza kumzidi mwenzake akimkata na kumtupa chini.

Curious to see, lile tumbo la Elon.
Hapo mwisho😂. Ukiwa na tumbo mwanaume unazaraulika sana.

Yote kwa yote Elon akimkamata Mark atamuua
 
Mabilionea Elon Musk na Mark Zuckerberg wamenuia kutoana jasho ndani ya ulingo baada ya wawili hao kuthibitisha kila mmoja.

Elon Musk Boss wa Twitter, Kampuni ya Tesla na SpaceX ameomba pambano dhidi ya mwenzake Mark Zuckerberg mmiliki wa Instagram na Mwanzilishi wa Facebook ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Meta.

Elon Musk tajiri namba moja Duniani alimtaka Mark Zuckerberg wakutane ulingoni baada ya boss huyo wa Facebook kutangaza nia yake ya kuunda mtandao wa kijamii utakaoleta ushindani na Twitter.

Bila ajizi Mark Zuckerberg mwenye umri wa miaka 39 alimjibu bilionea mwenzake Elon Musk (51) ataje mahala watakapo pambania na ndipo kujibiwa kuwa ni Vegas Octagon.

Vegas Octagon ni ulingo unaotumika kwa mapambano ya Ultimate Fighting Championship (UFC) unaopatikana Las Vegas, Nevada.

Elon Musk tajiri namba moja (1) duniani akiwa na mkwanja wenye thamani ya jumla dola bilioni 239.5 huku Mark Zuckerberg akiwa na bilionea namba tisa (9) akiwa na utajiri wenye thamani ya dola bilioni 101.1

Nani ataibuka mshindi ulingoni..?
FB_IMG_16875111527970487.jpg


FB_IMG_16875110805989233.jpg
 
Elon Musk nahisi atapigwa kwa factor ya Umri pamoja na Ubonge alionao.

Najua wale walionunua Midoli yake ya kike lazima waje wamtetee 🤪🏃🏃
 
Na mimi nikiwa na hela ntapigana na mwenye hela mwenzangu😅 Ata kama ni wilayani sawa
 
Waamerika wao ili uoneshe kuwa kidume kwa mwenzio mnamalizana ulingoni kisha mnapeana mikono na tabasamu kila mmoja anaenda kuuguza ngeu zake...
Sisi huku ukijichanganya ni kuchukuliana mademu!!
 
Back
Top Bottom