Natabiri msimu huu Simba kuchukua ubingwa tena, Azam kushika nafasi ya pili ligi kuu ya Tanzania

1. Simba
2. Azam
3. Biashara
4. Ruvu ya Masau Bwire
5. KMC
6. Namungo
7. Coastal Union
Sidhani kama kuna timu kubwa nimeisahau hapa
Da hatakama dharau kwa Chura FC siyo hivyo aisee,hapana mwaka huu watapambana sana azamu nafasi ya pili hamna.
 
Tunaomba utabiri wako kuhusu Yanga watapigwa kuanzia magoli mangapi kule Kwa kina Boko Haram?
Kama wenyewe Rivers wamesema watawachapa 4 sisi ni akina nani hadi tuwabishie?

Ila Rivers wanna dharau wale watu, yaani pamoja na yanga kujidai wamesajili sana lakini jamaa wanasema walicheza kama watoto.
 
Tena dharau kubwa mno,hivi msemaji mpya wa mabingwa wa kihistoria yupo nchini au amesafiri?
 
Mkuu utabiri wako unaweza kuwa wa kweli, lakin ni mapema kuweka bayana hilo! Ujue pamoja na usajili iloufanya pia Simba imeondokewa na wachezaji mahiri kama Triple C na Konde Boy! Ni wachezaji ambao tayri walikuwa wameshajenga muunganiko ambao kuujenga kwa haraka sio jambo jepesi!
Jambo la kuomba Mungu ni waanze vizuri ligi kuu na CAF champions Lg, wakichemsha hapo migogoro ni lazima itaibuka klabuni!
Yanga safari hii wamefanya usajili mkali, tusiwachukulie poa!
Kweli wamefanya usajili mkali, wote tuliona hilo siku ya kilele cha wiki ya mwananchi na juzi pale taifa dhidi ya Rivers.. Nasema uongo ndugu zangu?
 
Simba bingwa tena msimu huu wa 2021/2022. Azam atashika nafasi ya pili.

Kimataifa Simba itavuka hatua ya makundi klabu bingwa CAFCL.
Mkuu hapa umetumia hisia kuliko reality.

Em fanya 'homework' yako tena vizuri.
 
Kweli wamefanya usajili mkali, wote tuliona hilo siku ya kilele cha wiki ya mwananchi na juzi pale taifa dhidi ya Rivers.. Nasema uongo ndugu zangu?
Mkuu hizi mechi 2 walizocheza Yanga na kupoteza, haziwezi kutoa picha ya kusema moja kwa moja Simba tutachukua ubingwa!
Ukiangalia ile mechi ya awali(Yanga Day), Walicheza na timu yenye muunganiko bora kabisa , alafu wao wakawa bize kubadilisha wachezaji ili kutoa nafasi ya kila mmoja kuonyesha uwezo wake kwa mashabiki ikiwa ni sehemu ya utambulisho.
Mabadiliko ya aina ile ni lazima yataathiri timu na kama mpinzani mnayecheza nae ana kikosi kizuri ni lazima apige goli.
Pia kwenye hii mechi ya juzi dhidi ya Rivers united, Yanga waliingia uwanjani wakiwa tayari wameshavurugwa kisaikolojia na mambo mawili, Jambo la kwanza ni kocha wao kuanza kujitetea kuhusu muunganiko wa timu na kuonyesha wasiwasi wa kushinda!
Jambo la pili ni kitendo cha wachezaji wake kadhaa ambao Yanga iliamini wangekuwa na msaada kwa timu katika mechi ile lakini wakazuiwa kucheza na kufanya Yanga wabaki wakihangaika na suala lao hadi siku ya mchezo, hapa ni dhahir hawakuwa na plan B ya haraka!
Binafsi pamoja na kuwa shabiki wa Simba bado naona Yanga inaweza kufanya vizuri zaidi hasa wakiachana na mpira wa maneno mengi na kuanza kucheza soka la uwanjani!
 
Umeongea maneno mengi halafu yanaji contradict yenyewe hadi nashindwa nikujibu kipi niache kipi.

Ila Yanga ni ile ile jana, leo na hata kesho. Kama watabadilika ni miaka mingi ijayo mana hawana huo mpango kwa sasa. Timu kubwa zinaachana na uswahili wao ndo wanaukaribisha na kuudumisha.
 
Kuhusu Simba kuchukua ubingwa wa ligi ya bongo huo sio utabiri,ni mkakati wa Simba uliowekwa zaidi ya miaka minne nyuma.
Weka bayana msimu huu kwenye klabu bingwa caf Simba atafika fainali au hafiki?
 
Mkuu utabiri wako unaweza kuwa wa kweli, lakin ni mapema kuweka bayana hilo! Ujue pamoja na usajili iloufanya pia Simba imeondokewa na wachezaji mahiri kama Triple C na Konde Boy! Ni wachezaji ambao tayri walikuwa wameshajenga muunganiko ambao kuujenga kwa haraka sio jambo jepesi!
Jambo la kuomba Mungu ni waanze vizuri ligi kuu na CAF champions Lg, wakichemsha hapo migogoro ni lazima itaibuka klabuni!
Yanga safari hii wamefanya usajili mkali, tusiwachukulie poa!
Zipo mechi Simba walipata matokeo bila Chama na Merquisone.
Wachezaji wapya Simba walipitisha chekecheo kwa kina sana mpaka kuwapata hawa wachezaji wa kuwarithi Chama na Merqueosone hivyo ondoa shaka kwenye hilo.

Kuhusu Simba ikitolewa hatua ya awali kutazuka mgogoro,hilo sahau kutokea hata kama Simba ikitolewa hatua za awali.mashabiki wa Simba na uongozi wao washapevuka kwenye maswala ya soka na ni wavumilivu ukilinganisha na majirani zao wakuu ambao wanataka mafanikio ya haraka.
 
Back
Top Bottom