Habari wanandugu,
Miezi kadhaa iliyopita niliweka uzi hapa uliosomeka "
NATAFUTA BUSINESS PARTNER". Biashara hii inadeal na Engineering Works. Katika uzi huu nilianisha juu ya changamoto kubwa niliyonayo ambayo ni uhitaji wa machine za kufanyia kazi ambazo ni
LATHE MACHINE, MILLING MACHINE, SLOTING MACHINE na POWER SAW MACHINE.
Baada ya kufanyia kazi ushauri niliopewa na wadau kwenye uzi wangu wa kwanza. Baadae niliweka uzi mwingine unaosomeka
"LATHE MACHINE". Hapa niliandika natafuta mtu au kampuni inayoweza kunikodishia LATHE MACHINE kwa gharama ndogo, au kuniuzia hiyo LATHE MACHINE kwa malipo ya Installment ( Niwe nalipa kidogo kidogo hadi pale nitakapo maliza kulipa deni).
Katika kupambana na hili, nimepata mdau anaeuza LATHE MACHINE yake kwa gharama ya shilingi Milioni nane (Tsh. 8M) na fedha hiyo anaitaka yote kwa pamoja. Kwa hali yangu ya sasa sina uwezo huo wa shilingi Milioni 8 (Japokuwa mimi ni Engineer, mwenye experience ya zaidi ya miaka 4 toka nitoke chuo).
Wakuu, mimi kijana ninakuja kwenu kuomba msaada niweze kupata LATHE MACHINE tu, hizo machine nyingine nina amini 101% zitanunuliwa na hiyo LATHE MACHINE pindi biashara ikitengamaa. Wewe kama kijana mwenzangu (mzazi wangu) nina omba unishike mkono kwenye hili, unaweza kunisaidia kwa njia zifuatazo:
1. Kuninunulia hiyo LATHE MACHINE, mimi nikawa nazirudisha hizo hela zako pole pole pamoja na riba.
2. Ukaniunganisha na mtu au kampuni ambayo inaweza kunikopesha LATHE MACHINE na nikawa narejesha mkopo kwa gharama nafuu.
N.B
Mimi ninachohitaji ni Machine na sio hela.
Picha ya LATHE MACHINE (6ft) ambayo inauzwa 8M.
View attachment 1791466
Naomba nitangulize shukrani. Na Mungu aendelee kuwabariki.