Natafuta Business Partener

Natafuta Business Partener

Mkuu hata mimi natamani kama ningeweza kupewa mkopo na bank. Lakini si unajua bank hawatoi mkopo mpaka uwe na Asset
Kuna jamaa wanakopesha mashine (sina uhakika) na hio machine inakua ndio dhamana.
 
Hii Lathe Machine ya mwaka gani? Mbona imechoka sana?

Kila la kheri katika hitaji lako...
 
Hii Lathe Machine ya mwaka gani? Mbona imechoka sana?

Kila la kheri katika hitaji lako...
hyo ni used mkuu ndio maana bei yake ni ndogo. Lathe machine mpya bei yake ni kubwa sana, inacheza around $150,000 hadi 300,000 (Hizi ni zile ambazo ni heavy duty)
 
Agiza China, utapata kwa almost nusu ya hio bei lakini utasubiri 45 - 60 days kuipata
Kuna gharama za usafirishaji na gharama za kulipia bandarini. Kitu ambacho utakuta price imerudi huko huko.

Halikadharika changamoto yangu kubwa kwa sasa hivi ni kwamba sina hyo hela ya kununua au kuagiza hyo machine
 
ni bora kuanza na used inapatikana hela ya kununua mpya mda sio mrefu najua hii deal
 
Chris lukosi ndio shuguli zake hizi za vifaa kama huyu mwamba hapa
 
Niko Dar mkuu
Mkuu naomba Mungu akusaidie ufanikishe, sina uwezo wa kifedha ila nataman sana ningekua business partner/assistant wako kwan na mimi nimesomea fani hio ingawa sina uzoefu sana
 
Habari wanandugu,

Miezi kadhaa iliyopita niliweka uzi hapa uliosomeka "NATAFUTA BUSINESS PARTNER". Biashara hii inadeal na Engineering Works. Katika uzi huu nilianisha juu ya changamoto kubwa niliyonayo ambayo ni uhitaji wa machine za kufanyia kazi ambazo ni LATHE MACHINE, MILLING MACHINE, SLOTING MACHINE na POWER SAW MACHINE.

Baada ya kufanyia kazi ushauri niliopewa na wadau kwenye uzi wangu wa kwanza. Baadae niliweka uzi mwingine unaosomeka "LATHE MACHINE". Hapa niliandika natafuta mtu au kampuni inayoweza kunikodishia LATHE MACHINE kwa gharama ndogo, au kuniuzia hiyo LATHE MACHINE kwa malipo ya Installment ( Niwe nalipa kidogo kidogo hadi pale nitakapo maliza kulipa deni).

Katika kupambana na hili, nimepata mdau anaeuza LATHE MACHINE yake kwa gharama ya shilingi Milioni nane (Tsh. 8M) na fedha hiyo anaitaka yote kwa pamoja. Kwa hali yangu ya sasa sina uwezo huo wa shilingi Milioni 8 (Japokuwa mimi ni Engineer, mwenye experience ya zaidi ya miaka 4 toka nitoke chuo).

Wakuu, mimi kijana ninakuja kwenu kuomba msaada niweze kupata LATHE MACHINE tu, hizo machine nyingine nina amini 101% zitanunuliwa na hiyo LATHE MACHINE pindi biashara ikitengamaa. Wewe kama kijana mwenzangu (mzazi wangu) nina omba unishike mkono kwenye hili, unaweza kunisaidia kwa njia zifuatazo:

1. Kuninunulia hiyo LATHE MACHINE, mimi nikawa nazirudisha hizo hela zako pole pole pamoja na riba.

2. Ukaniunganisha na mtu au kampuni ambayo inaweza kunikopesha LATHE MACHINE na nikawa narejesha mkopo kwa gharama nafuu.

N.B
Mimi ninachohitaji ni Machine na sio hela.


Picha ya LATHE MACHINE (6ft) ambayo inauzwa 8M.View attachment 1791466


Naomba nitangulize shukrani. Na Mungu aendelee kuwabariki.
Nakushauri uwende kwenye Halmashauri y'ako Idara ya Maendeleo ya Jamii inayohusika na mikopo ya 10% KWA Vijana 4%, Wanawake 4% na Walemavu 2%.

Waone na kuwapatia wazo Lako na likiwa limeanisha kila kitu. Ninauhakika watakusaidia kwasababu wazo Lako ni zuri na litaongeza ajira KWA Vijana wengine.

Waweza kunicheki PM kwa maelezo zaidi.
 
Back
Top Bottom