Natafuta Caterpillar la kusafisha shamba jipya (pori)

Natafuta Caterpillar la kusafisha shamba jipya (pori)

Mr Confidential

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,532
Reaction score
2,415
Wakuu natumai mu-wazima wa afya,

Natafuta Caterpillar la kuvunja shamba. Shamba lipo mkoa Pwani (km 160 kutoka Dar).

Ningependa kujua gharama ya kukodisha, kusafirisha na kama Kuna gharama zingine
 
Attachments

  • Bulldozer.jpg
    Bulldozer.jpg
    66.7 KB · Views: 19
Wakuu, mwenye kufahamu kuhusu haya macaterpillar naomba anisaidie
 
Wakuu natumai mu-wazima wa afya,

Natafuta Caterpillar la kuvunja shamba. Shamba lipo mkoa Pwani (km 160 kutoka Dar).

Ningependa kujua gharama ya kukodisha, kusafirisha na kama Kuna gharama zingine
Kuna caterpillar na tractor za kulimia, kwani wewe unataka caterpillar wataka kutengeneza barabara ndani ya shamba???
 
Kuna caterpillar na tractor za kulimia, kwani wewe unataka caterpillar wataka kutengeneza barabara ndani ya shamba???
Nilivyomuelewa anahitaji kusafisha shamba kama kung'oa miti visiki nk.
 
Taja eneo ni wapi wenye makatapila upande huo waje waangalie shamba lilivyo kwanza na uzito wa kazi yenyewe na landscape yenyewe ilivyo barabara za kufika huko ,kwaweza kuwa na mito na mabonde,Majabali,matope nk kufika huko nk lazima assessment ifanyike kwanza weka details watu waje kwanza kuona

Umetoa information shallow sana
 
Nilivyomuelewa anahitaji kusafisha shamba kama kung'oa miti visiki nk.
Liko wapi caterpillar huwa haiondoki tu bila engineer kuja kuangalia eneo na kuona gharama zitatumika na mafuta yatatumika kiasi gani na kazi ina ukubwa gani
 
Wakuu natumai mu-wazima wa afya,

Natafuta Caterpillar la kuvunja shamba. Shamba lipo mkoa Pwani (km 160 kutoka Dar).

Ningependa kujua gharama ya kukodisha, kusafirisha na kama Kuna gharama zingine
Zipo,ukubwa wa eneo lako ni ekari ngapi?
Geography ya eneo ikoje,na msitu wako upoje pia?,
Gharama ni 100,000/hr,kwa siku linafanya kazi 8hrs,
Gharama za Operator ni zako Tsh 50,000/day bila gharama za malazi,
Diesel ni ya kwako @100ltrs/day,
Inaweza chakata ekari 3-7 kwa siku,
Gharama za kuileta na kuirudisha ni ya kwako,@2,400,000 kwenda na kurudi.
 
Vizuri umeelezea kila kitu mkuu
 
Nipo Manyoni Singida, Mimi pia Nimenunua heka 50 shamba pori lakn gharama za kusafisha kwa greda ni kubwa mara 4 zaid ya kununua eneo.
Wahusika wa greda waliniambia
Mafuta Lita 24 kwa saa na linafanya Kaz masaa 8, opereta nimlipe Mimi 80000tsh kwa siku, gharama ya usafiri kwenda na kurud ni 1000000tsh na malipo kwa mmiliki wa chombo/greda ni 1000000tsh kwa siku
 
Back
Top Bottom