Madalali hawajaona hili tangazo? Jaribu ku-gugu (in Makala's voice) Dalali wa nyumba Mwenge. Utapata orodha ya madalali. Ila umekosea iutaja budget yako, madalali watachezesha humo humo!Wakuu, natafuta nyumba ya kupanga self-contained kiwe chumba kimoja na sebule. Maeneo ya Mbezi Africana kurudi mpaka Mwenge na Kawe. Isiwe mbali na barabara kuu. Meter ya maji na Luku ya umeme kujitegemea. Itapendeza ikiwa ndani ya geti na yenye sehemu ya kuegesha magari ndani.
Budget yangu ni kuanzia laki 2 mpaka laki 3 kwa mwezi, na uwezo wa kulipa miezi sita sita upo. Kuhamia wiki ijayo ya June 8 na kuendelea. Msaada tafadhali kwa mwenye connection
Natanguliza shukrani zangu. Asanteni
Tumezunguka sana, bila mafanikio. Halafu wengine wanasema washawapa majukumu madalali. Ukienda kwa madalali wanakupeleka nyumba ambazo sio zinazokidhi criteria zako. Ni shida tu. Ndiyo maana nikaleta jukwaani labda kuna mwanachama ana nyumba zake anaweza pangisha, rather than kupitia madalali au kutumia muda mrefu kuzunguka wilaya ya kinondoni nzima. But shukran kwa ushauriUkitafuta nyumba ya kupanga nenda maeneo husika ukiweza unawauliza wenyeji kabla ya kukutana na hao Maagent kuwa haya mazingira mnapangisha kissing gani kwa nyumba yenye vyumba kadhaa ndio utapata kitu bora mambo ya kutumia mtandao ni baada ya manual kushindikana na huku una taarifa zote hata kununua kiwanja wasizwa wanatumia hii minutes ya Mzee Mkwawa au Kinjekitile Ngwele..
Tumewatumia madalali sana but nyumba wanazokupeleka wanasema iko karibu na barabara. Ila, ziko mbali na hiyo barabara sasa ya kufika kwenye nyumba, ni balaa. Ukifika nyumba nzuri, lakini hakuna maji, na bado inakarabatiwa. Anyways nitajaribu tena leo na weekend hiiMadalali hawajaona hili tangazo? Jaribu ku-gugu (in Makala's voice) Dalali wa nyumba Mwenge. Utapata orodha ya madalali. Ila umekosea iutaja budget yako, madalali watachezesha humo humo!