Natafuta gari aina ya funcargo!!

Natafuta gari aina ya funcargo!!

Ukishaelewa kitu kinachoitwa upendo kinavyofanya kazi, basi utagundua anayeipenda Funcargo na anaueiponda, wote wapo sahihi....

Si kila unachokipenda kitapendwa na kila mtu...
Magari ni kama nguo,... T-shirts yako unayoiona ni kali sana, kuna mtu kwake ni dekio tu..

Magari ni kama wanawake, huyo mwanamke wako unayemuona ni pisi kali, classic, kuna watu wanamuona kinyago tu...

Kila mtu ana ladha yake, tumsapoti tu anayeipenda funcargo....ndiyo taste yake imeangukia hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Funcargo ...the best car KATIKA gati hizi ndogo inaspace kubwa sana ndani .... Kuliko hata IST .......Bora funcargo kuliko port au sienta even vitz ...Mimi binafsi Nina Funcargo naipenda sana ... Pia itambuliwe kila mtu ana intrest yake hata ukimiliki Hammer inachangamto zake so kisikutishe kitu as long as spear zipo nyingi za Toyota tena Affordable ...usiogope kabisa
Kati ya sienta na funcargo hapo mi naona bora sienta
 
Wanaoiponda Fun cargo wengi wao hawa hapa..[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]..
images.jpg
 
Spacio, IST, Ractis, Runx...... Hizo zina shape nzuri
Nakuunga mkono na mguu fancargo hapana Kuna jirani yangu hapa anako kana shape mbaya Kama ilivyo tactic nayo hapana kwa upande wangu lakini chagua Kati ya hizo alizokutajia mdau hapo juu hutojuta badas

Mimi nilinunua vits nilinuta baada ya miezi miwili tu baada ya kupakia mabonge watatu nilishindwa kupanda mlima mdogo tu mpaka nikawashusha nikapanda mwenyewe nikawasubiri kwa mbele
 
Hiyo vitz yako itakuwa ilikuwa na fuel pump mbovu
 
Salaam,

Toyota Funcargo ni moja kati ya magari yenye sifa kubwa kabisa kutoka kwenye kampuni ya toyota. Sifa hio nayo ni utumiaji mdodo wa mafuta.

Hizi gari kwakweli zinasifika sana juu ya upande huo wa matumizi madogo ya mafuta, infact kuliko kununua vitz, ni bora hizi. Maana ina nafasi ya kutosha kabisa ndani, na kikubwa zaidi zile siti (za nyuma ) unaweza kuzilaza na ukapata nafasi kubwa zaidi kuweza kuwekea vitu.

MATATIZO YAKE ;

Hakuna gari ambayo hinga matatizo, kila gari inaudhaifu wake.

Hizi gari, udhaifu wake ni;

Shock absobers
Bushes
Bearing

Lakini pamoja na hayo yote, upatikanaji wa spare parts zake ni mkubwa sana, spare parts zake ziko kwa wingi mno.

Ikiwa utahitaji, karibu tuwasiliane. Kwa Tshs 8,500,000 ninaweza kukuletea kutoka japan, mpaka kukabidhi mkononi , utakacholipia ni bima tu basi.

Ahsante
Ilinibidi nirudi kuangalia tarehe hasa baada ya kuona bei ya 8.5M ila nikawaza juu ya waraka wa Dr. Philip Mpango😂 juu ya kikokotoo cha dharura 2021
 
Daah, wadau mmenipa ngumu nyingi sana za usoni......
Anyway ni kweli FunCargo ina sura nzuri ingawa wengine mnaona mbaya.
Uzuri na ubaya uko machoni pa mtazamaji.

Naomba mnisaidie kiufundi zaidi kuliko kimuonekano.
Kulikoni hio Funcargo ni aheri Toyota Sienta kwa kweli japo nacho kimekaa hivyo hivyo ila kina make sense.
 
Funcargo ...the best car KATIKA gati hizi ndogo inaspace kubwa sana ndani .... Kuliko hata IST .......Bora funcargo kuliko port au sienta even vitz ...Mimi binafsi Nina Funcargo naipenda sana ... Pia itambuliwe kila mtu ana intrest yake hata ukimiliki Hammer inachangamto zake so kisikutishe kitu as long as spear zipo nyingi za Toyota tena Affordable ...usiogope kabisa
Japo hizo gari zote sizikubali ila i would go for sienta atleast ina unafuu kwenye macho yangu.
 
Habari za asubuhi wadau,

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, nahitaji funcargo ingawa bajeti yangu ya 5M ni ndogo lkn ndio nahitaji gari hiyo iwe kuanzia namba C iliyo karibu na D na kuendelea.

Wadau mie hiyo ndio itakua gari yangu ya kwanza, sijawahi kumiliki gari hivyo mwenye nalo tafadhali tuwasiliane, pamoja kuwa ndilo gari ninalohitaji pia nakaribisha maoni au msaada zaidi wa mawazo ya gari ipi ni nzuri kutokana na bajeti yangu hiyo.

Passo nilikua naipenda lkn kutokana na maoni ya kitaalamu niliyoyasoma humu naona passo haitanifaa kwa kazi zangu za humu mjini lkn pia na kwenda mikoani.

Pia nitashukuru sana kama nitapata uzuri na ubaya wa funcargo.

Natanguliza shukrani.
Unapeleka wapi sasa nawewe?
 
Watu oooooo...... watu eeeeee.... watu o kwahiyo funcargo ulinunua ama maneno ya watu yalikukwamisha kwene reli??
 
Watu oooooo...... watu eeeeee.... watu o kwahiyo funcargo ulinunua ama maneno ya watu yalikukwamisha kwene reli??
Mimi niliiagiza mwaka jana mwezi wa pili iko poa sana na siijutii , nimefunga sports rims, muziki mkubwa wa Android na woofer kubwa double coil la pioneer huwezi amini kila nikipita watu lazima waitolee macho
 
funcargo ina shepu mbaya, alafu haipo imara! kiukwel sikushauri ununue funcargo
  • kama unataka ya cc ndogo chukua vitz utafurah na roho yako, ni ngumu na zinavumilia shida zote
  • kama unataka gari yenye cc ndogo na ipo juu basi chukua Ractis
Ractis ya mil 5 ipo?
 
Back
Top Bottom