Natafuta gari aina ya funcargo!!

Ukishaelewa kitu kinachoitwa upendo kinavyofanya kazi, basi utagundua anayeipenda Funcargo na anaueiponda, wote wapo sahihi....

Si kila unachokipenda kitapendwa na kila mtu...
Magari ni kama nguo,... T-shirts yako unayoiona ni kali sana, kuna mtu kwake ni dekio tu..

Magari ni kama wanawake, huyo mwanamke wako unayemuona ni pisi kali, classic, kuna watu wanamuona kinyago tu...

Kila mtu ana ladha yake, tumsapoti tu anayeipenda funcargo....ndiyo taste yake imeangukia hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kati ya sienta na funcargo hapo mi naona bora sienta
 
Spacio, IST, Ractis, Runx...... Hizo zina shape nzuri
Nakuunga mkono na mguu fancargo hapana Kuna jirani yangu hapa anako kana shape mbaya Kama ilivyo tactic nayo hapana kwa upande wangu lakini chagua Kati ya hizo alizokutajia mdau hapo juu hutojuta badas

Mimi nilinunua vits nilinuta baada ya miezi miwili tu baada ya kupakia mabonge watatu nilishindwa kupanda mlima mdogo tu mpaka nikawashusha nikapanda mwenyewe nikawasubiri kwa mbele
 
Hiyo vitz yako itakuwa ilikuwa na fuel pump mbovu
 
Daah, wadau mmenipa ngumu nyingi sana za usoni......
Anyway ni kweli FunCargo ina sura nzuri ingawa wengine mnaona mbaya.
Uzuri na ubaya uko machoni pa mtazamaji.

Naomba mnisaidie kiufundi zaidi kuliko kimuonekano.
 
Ilinibidi nirudi kuangalia tarehe hasa baada ya kuona bei ya 8.5M ila nikawaza juu ya waraka wa Dr. Philip MpangoπŸ˜‚ juu ya kikokotoo cha dharura 2021
 
Daah, wadau mmenipa ngumu nyingi sana za usoni......
Anyway ni kweli FunCargo ina sura nzuri ingawa wengine mnaona mbaya.
Uzuri na ubaya uko machoni pa mtazamaji.

Naomba mnisaidie kiufundi zaidi kuliko kimuonekano.
Kulikoni hio Funcargo ni aheri Toyota Sienta kwa kweli japo nacho kimekaa hivyo hivyo ila kina make sense.
 
Japo hizo gari zote sizikubali ila i would go for sienta atleast ina unafuu kwenye macho yangu.
 
Unapeleka wapi sasa nawewe?
 
Watu oooooo...... watu eeeeee.... watu o kwahiyo funcargo ulinunua ama maneno ya watu yalikukwamisha kwene reli??
 
Watu oooooo...... watu eeeeee.... watu o kwahiyo funcargo ulinunua ama maneno ya watu yalikukwamisha kwene reli??
Mimi niliiagiza mwaka jana mwezi wa pili iko poa sana na siijutii , nimefunga sports rims, muziki mkubwa wa Android na woofer kubwa double coil la pioneer huwezi amini kila nikipita watu lazima waitolee macho
 
funcargo ina shepu mbaya, alafu haipo imara! kiukwel sikushauri ununue funcargo
  • kama unataka ya cc ndogo chukua vitz utafurah na roho yako, ni ngumu na zinavumilia shida zote
  • kama unataka gari yenye cc ndogo na ipo juu basi chukua Ractis
Ractis ya mil 5 ipo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…