Natafuta internship au kazi pale nitakapo maliza Diploma 2 in computer science. Au constructive criticism

Status
Not open for further replies.
Upo vizuri puuza comments zinazokukatisha tamaa. Kuna wajuaji wengi humu.

Nimeona page yako ya portfolio kuna animations video na app pia nimeona, kama bado chuo Anza kuzipush project zako sasa hivi usisubiri umalize chuo.

Kwa mfano animations za hadithi za Kiswahili zipo chache YouTube, ukianza kuzitengeneza upload YouTube na uikuze channel yako Kwa muda WA mwaka mmoja mpaka miwili.

Kama utakuwa serious Kwa kipindi hiko utaanza kuingiza chochote kitu.

Na pia unaweza tumia video zako kuomba kazi za Motion Graphics kwenye website ya Upwork.

Pia achana na free web hosting kama una hela nunua server na domain(sio bei kubwa) fungua website na uitumie web yako kutangaza application yako.

Kwenye application pia fikirie kuongeza virtual good(in app purchase) na pia tengeneza app au website inayotarget mataifa ya nje(UK, USa, Canada, Australia nk) Kwa sababu hao angalau wako tayari kununua services zinazouzwa na app.

Na inabidi ujifunze ASO(App store optimization) na SEO(Search Engine Optimisation) na digital market zingine Kwa sababu kuwa na product bila kuwa na watumiaji ni upotezaji WA muda.

Ukiyafanya haya sasa utapata experience kubwa na wala hutohitaji kujitolea Kwa mtu.

Wapuuze kabisa wanakwambia usubiri kumaliza chuo.
 
Una haraka ya nini, au lengo lako msoto wa ajira usukukumbe? Kama unapenda sana unachofanya na hupendi kukaa idle basi jiajiri mwenyewe.
 
Dah maneno mazuri sana mkuu na umenifumbua macho kwenye mambo mengi. Nitayafanyia kazi. Asante sana.
 
Nathani ungeweka contact ingerahisisha kuwa connected na wenye internships / ajira
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…