Natafuta kazi, kama sio ya kulipwa basi hata kujitolea

Natafuta kazi, kama sio ya kulipwa basi hata kujitolea

..
Sema ni ufala sana mtu uwe na sifa zako ulizozisotea school alafu uje street uanze kutia huruma me ndo maana shule sijutii kuishia njiani maana nimejifunza kwamba wasomi wengi wana limit kwenye fikira zao, wanaamini kuajiriwa na kulipwa ndo goals zao. Wakati me nikipiga jicho naona i can be anyone i want, i can own anything i want, simpaparikii yoyote na wala simsujudii yoyote wote naona sawa tu… kiufupi sioni limit kwangu naona nahitaji tu ubunifu kidogo na uthubutu then nianze kujipimia mihela tu.

Hujutiii ila bila shaka uliumia sana ulipoishia njiani, wewe na Doto Magari hamna tofauti sana.
 
Business IT kbs hapa kunakitu hakipo sawa futa mawazo ya kwamba unaelimu fanya kazi yyt
 
Mwenye kampuni au biashara binafsi, kwa elimu yako, unawezaje kumsaidia kupata mapato zaidi?
 
Kwa uhalisia yaonesha una elimu ila hujaelimika.
Una profile nzuri ila kuitumia ndiyo tatizo.
Usipende laumu kubebwa, hakuna wa kumbeba mtu, hata huko serikalini mambo yamebadilika.

Kwa profile yako nenda machinga complex jifunze vitu na usijiweke msomi.

Afu usichague kazi
 
Hongera babaa.
Acha niendelee na ufala wangu huu huu humu. Kila mtu ana umuhimu wake katika eneo husika.
Hata mimi leo hii najiuliza, hivi watu wote wangesoma, akina nani wangekuwa wanatuchomea mahindi mtaani? Ila jibu nimepata.
Hongera sana mkuu.
Wanaochomelea mageti ndo unaona hawajasoma sio? 😁😁😁 kwa hizo akili zako bado hujajua maisha ni nini haya tafuta ajira blud
 
Jamani ndugu zangu, wenye makampuni, viwanda au wenye ndugu, marafiki na wadau.

Naomba kazi hata ya kujitolea nipate angalau experience ya kazi.. Nipo tayari kujitolea jamani, maana nikienda directly kuomba kazi na kupereka Cv narudishwa punde tu nikifika mapokezi, naambiwa nafasi hazipo hapa na hatuchukui intern. Kazi zetu tunatanganza kwenye ajira portal.

Mimi ni fresh graduate. Nina degree ya Business IT.
Naweza kufanya kazi za database administration (mySQL database, mariaDB Ubuntu server configuration?, business analysis, Business Intelligence, Business Process management, customer relationship management.

Pia nina basic knowledge ya Cyber security, advanced knowledge in LINUX
Pia nipo tayari kufanya kazi yoyote nitakayopewa na kampuni tofauti na mambo niliyosomea.

Nipo Dar es salaam. Ubungo RiverSide.

Mawasiliano; Normal call: 0616604372
Whatsap: 0620224372.
Jamani mnisaidie, sina pakuenda, sina ndugu yeyote anayefanya kazi serikalini walau wa kunisaidia kutafuta hata nafasi ya internship.

Msaada wenu wakuu wangu, familia inanitegemea kama msomi wa nyumbani, japo ndo nimemaliza chuo. Nyumbani patupu.
Nimekuelewa mnoo, nilipitia changamoto kama izo uko nyuma ila nashukuru mungu kwa sasa kidogo mambo yame settle.
Jaribu kufanya ivi ~:
1).chukua computer yako kama ni laptop nunua kioo lipana cha desktop thn tafuta vispika fungua sehemu anza kuuza zile movie/series za mitahani na andika bango kua una frash na simu hapohapo uza na vichaji, earphone, flash na vitu vyengine vidogo vidogo.

2). Tenga siku hata mara tatu kwa week pitia katika izi shule ambazo bado sio kubwa maana shule nyingi hazina budget za kumuajili mtu wa IT kwao wana focus luajili walimu kwasababu wana direct impact kwao ukifika uko uwe na kipeperushi chenye taharifa unazozifanya base katka hardware, graphics na website design uko usiende kwa style ya kuomba kazi nenda kama mtu ambae unaweza ukatatua changamoto zao wakakulipa na mkamaliza.

NB. Jitahid uwe mwaminifu sana kwa kila kazi ambayo mungu ataileta katika mikono yako, mfanye mteja baada ya kukutana na ww asifikilie kwenda kwa mtu mwengine kwa huduma ambayo ww unaweza ukampa.

Mwisho endelea kupambania ajira kote kote serikali na private sector na jitahid pambania sana izi za ajira portal kwan uku hakuna kujuana mwenye msuri wake anatoboa..

Pambana kuna siku utakua unawasimulia watu ayo unayopitia kama story tena uku ukiwa unacheka..
 
Back
Top Bottom