Natafuta kazi, kama sio ya kulipwa basi hata kujitolea

..
Hujutiii ila bila shaka uliumia sana ulipoishia njiani, wewe na Doto Magari hamna tofauti sana.
 
Business IT kbs hapa kunakitu hakipo sawa futa mawazo ya kwamba unaelimu fanya kazi yyt
 
Mwenye kampuni au biashara binafsi, kwa elimu yako, unawezaje kumsaidia kupata mapato zaidi?
 
Kwa uhalisia yaonesha una elimu ila hujaelimika.
Una profile nzuri ila kuitumia ndiyo tatizo.
Usipende laumu kubebwa, hakuna wa kumbeba mtu, hata huko serikalini mambo yamebadilika.

Kwa profile yako nenda machinga complex jifunze vitu na usijiweke msomi.

Afu usichague kazi
 
Hongera babaa.
Acha niendelee na ufala wangu huu huu humu. Kila mtu ana umuhimu wake katika eneo husika.
Hata mimi leo hii najiuliza, hivi watu wote wangesoma, akina nani wangekuwa wanatuchomea mahindi mtaani? Ila jibu nimepata.
Hongera sana mkuu.
Wanaochomelea mageti ndo unaona hawajasoma sio? 😁😁😁 kwa hizo akili zako bado hujajua maisha ni nini haya tafuta ajira blud
 
Nimekuelewa mnoo, nilipitia changamoto kama izo uko nyuma ila nashukuru mungu kwa sasa kidogo mambo yame settle.
Jaribu kufanya ivi ~:
1).chukua computer yako kama ni laptop nunua kioo lipana cha desktop thn tafuta vispika fungua sehemu anza kuuza zile movie/series za mitahani na andika bango kua una frash na simu hapohapo uza na vichaji, earphone, flash na vitu vyengine vidogo vidogo.

2). Tenga siku hata mara tatu kwa week pitia katika izi shule ambazo bado sio kubwa maana shule nyingi hazina budget za kumuajili mtu wa IT kwao wana focus luajili walimu kwasababu wana direct impact kwao ukifika uko uwe na kipeperushi chenye taharifa unazozifanya base katka hardware, graphics na website design uko usiende kwa style ya kuomba kazi nenda kama mtu ambae unaweza ukatatua changamoto zao wakakulipa na mkamaliza.

NB. Jitahid uwe mwaminifu sana kwa kila kazi ambayo mungu ataileta katika mikono yako, mfanye mteja baada ya kukutana na ww asifikilie kwenda kwa mtu mwengine kwa huduma ambayo ww unaweza ukampa.

Mwisho endelea kupambania ajira kote kote serikali na private sector na jitahid pambania sana izi za ajira portal kwan uku hakuna kujuana mwenye msuri wake anatoboa..

Pambana kuna siku utakua unawasimulia watu ayo unayopitia kama story tena uku ukiwa unacheka..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…