Mungu wangu!!! Hivi mpaka lini mtaelewa kwamba mambo ya kuungaunga ukitoka bachelor si mazuri? Unaona sasa, ulidhani ukipata masters ndio utapata kazi kirahisi na pia utalipwa zaidi ya mtu mwenye bachelor. Ungekuwa ulitokea kazini si ungerudi sasa kituo chako cha kazi? Ungekuwa umefungua miradi yako, si ungerudi sasa kuiendeleza? Umepoteza muda, kwa elimu ambayo hukuwa na uhakika kama itakusaidia kwenye soko la ajira.
Kwa kweli mimi sina huruma na watu style yako, tena napenda mteseke ili wengine wajifunze. Maisha siyo kushinda kusoma. Ukisoma degree ya kwanza au diploma yoyote unaingia katika ulimwengu wa kuajiriwa au kujiajiri then wasoma upepo huku na interests zako zikikuongoza kwa ajili ya masters kama unaona itasaidia kwa profession yako. Kumbuka unavyosoma zaidi ndivyo pia nafasi za kazi zinapungua, unaweza ukaenda kuomba kazi mahala na kuficha cheti ili upate kazi. Na pia ukiungaunga shule waajiri wengine wanakuogopa kwa kuwa watahitaji kukupa mshahara mkubwa kwa kitu usichoweza ku deliver au kwa kuwa huna experience nacho, yaani bado una utoto utoto wa shule. Halafu nyie wa kuunganisha bachelor kwenda masters huwa mnafikiria kuajiriwa kila siku. Huhitaji masters kufungua mradi wako binafsi. Shule ya duniani ni bora kuliko Msc yoyote. Angalia sasa usije ukaanza kukimbilia Phd. Maana wengine wanadhani maisha ni kusoma tu, utadhani unashindana na watoto wa fulani kijijini. Angalia sasa, usijeishia kuwa frustrated tu.