Natafuta kazi

RoadLofa

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2017
Posts
1,509
Reaction score
3,313
Ndugu zangu hadi kufikia hatua hii ninapitia kipindi kigumu sana. Kwanza kabisa mimi ni graduate wa Bachelor Degree in Accountancy, nina mwaka tangu nimalize nipo mtaani tu na umri wangu ni mkubwa zaidi ya miaka 30.

Kila nikiapply kazi mbalimbali zinazoendana na career yangu unakuta naenda kwenye interview unakuta nafaulu vizuri ila kazi nakosa, kwasababu watu wanapeana kwa connection. Hata kazi za sensa na postikodi nikaapply lakini sikupata kwa sababu zinatolewa kwa connection na mimi sina hiyo connection.

Kwa mtu yoyote ambaye anaweza kunisaidia kupata kazi popote inayoendana na course niliyosoma kama vile Accountant, Sales & Marketing etc iwe private au government institution hasisite kunijuza.
 
Kwanza tuanzie hapo,ni nani aliyekwambia kwenye hizo interview ulizoenda kufanya ilikuwa una faulu?au huwa unaenda kwenye usahili na matokeo yako?lakini pia thibitisha connection unayoisema watu hupeana tofauti na uwezo wako.
 
Do online bussiness.. ingia kwa vijana wenzako wajasirimali pambana nao.
Nguo... incubator... ufugaji... simu... kama ulivyofanya mtu anakuja kukushauri hapa.. hivo utapata wateja kutokana na product yako..uje unishukuru
 
Nenda mpanda katavi Kuna mapori makubwa kafyeke ulime ufuta na alizeti. Sasa wewe umekalisha makalio tu hapo kwa shemeji hutaki kutoka mjini uende mbwinde kutafuta fursa. Niushauri tu sikuzodogoi ila fursa zipo kijijini
 
Hayo mapori mpanda katavi y'ako sehemu Gani ambayo hayana watu (hayana umiliki) unafika unafyeka tu

Vp wakulima wa alizeti na ufuta mpanda wana hela sana maana imeonekana hicho kilimo huko kinalipa (naamini huna taarifa yoyote juu ya icho kilimo)
 
Nenda baa ya jirani ujitolee kuhudumia vinywaji
 
Nenda mpanda katavi Kuna mapori makubwa kafyeke ulime ufuta na alizeti. Sasa wewe umekalisha makalio tu hapo kwa shemeji hutaki kutoka mjini uende mbwinde kutafuta fursa. Niushauri tu sikuzodogoi ila fursa zipo kijijini
Kama hauwezi kumsaidia mtu angalao basi usimuumize zaidi, maisha ni kupanda na kushuka mkuu... be humble
 
Nenda mpanda katavi Kuna mapori makubwa kafyeke ulime ufuta na alizeti. Sasa wewe umekalisha makalio tu hapo kwa shemeji hutaki kutoka mjini uende mbwinde kutafuta fursa. Niushauri tu sikuzodogoi ila fursa zipo kijijini
Wewe jamaa nakuona(ga) kama mtu uliyekata tamaa na maisha na hujui ufanye nini. Unapenda sana kuwatukana wenzako bila sababu
 
Nenda mpanda katavi Kuna mapori makubwa kafyeke ulime ufuta na alizeti. Sasa wewe umekalisha makalio tu hapo kwa shemeji hutaki kutoka mjini uende mbwinde kutafuta fursa. Niushauri tu sikuzodogoi ila fursa zipo kijijini
Wewe jamaa nakuona(ga) kama mtu uliyekata tamaa na maisha na hujui ufanye nini. Unapenda sana kuwatukana wenzako bila sababu
 
Hayo mapori mpanda katavi y'ako sehemu Gani ambayo hayana watu (hayana umiliki) unafika unafyeka tu

Vp wakulima wa alizeti na ufuta mpanda wana hela sana maana imeonekana hicho kilimo huko kinalipa (naamini huna taarifa yoyote juu ya icho kilimo)
Hili nalo neno!!👌🏼
 
Nenda mpanda katavi Kuna mapori makubwa kafyeke ulime ufuta na alizeti. Sasa wewe umekalisha makalio tu hapo kwa shemeji hutaki kutoka mjini uende mbwinde kutafuta fursa. Niushauri tu sikuzodogoi ila fursa zipo kijijini
Sio lugha nzuri hata kama wewe una maisha mazuri. Umeshawahi kufika katavi? Je utafyeka pori la mtu au game reserve? Hiko kilimo utafanya bila mtaji? Umeshawahi kulima wewe? Atauza wapi? Mkuu sio kila mada ni ya kucomment, nyingine pita kimya tu mkuu kama hujaiona.
 
Wewe jamaa nakuona(ga) kama mtu uliyekata tamaa na maisha na hujui ufanye nini. Unapenda sana kuwatukana wenzako bila sababu
Ni kweli, anatakiwa abadilike. Ni kweli humu hatufahamiani ila unaweza mjua mtu kwa kile aandikacho. Muandiko umebeba utambulisho wa mtu. Huyu anaonekana ni "psychatric"
 
Unaona aje upite kwenye biashara binafsi, ujitambulishe na kuona ni jinsi gani utaweza kuwawekea vizuri mahesabu ya biashara zao?
 
Pole sana mkuu, piga moyo konde, endelea kupambana utapata tu.

Kila mmoja ana riziki yake ila njia ya kuipata hiyo riziki ndio zinatofautiana na ili uipate hiyo njia lazima upambane
 
unakuta naenda kwenye interview ila unakuta nafaulu vizuri ila kazi nakosa kwa sababu watu wanapeana kwa connection ata kazi za sensa na postikodi nikiapply lakini sikupata kwa sababu zinatolewa kwa connection na mimi sina iyo connection,
Unajuaje unafaulu vizuri, na umedhibitishaje Kuna konnekisheni!!!

Kwa hapa, inatia wasiwasi, maana unaweza kuwa mfanyamajungu Bora badala ya mfanyakazi Bora! Yawezekana waajiri wamekupima katika hili wakaona hufai.
===
Ushauri:
1. Ujikubali kwanza kuwa unaweza kufanya kazi yoyote Halali zaidi ya hiyo uliyosomea. Hapa namaanisha Hata kazi za kujiajili unaziweza na ambazo hukuzisomea mfano kuuza udogo wenye mbolea kwa ajili ya bustani, kuuza Maji, kufundisha twisheni na kadhalika.
2. Kubali kuwa kuna wakati mwingine unashindwa, na kushindwa siyo dhambi bali kunatumika kuboresha uwezo wako kwa kuongeza bidii na umakini wakati mwingine wa mashindano.
3. Achana kabisa na mawazo ya kuwa wanaopata nafasi wanapendelewa! Kama kweli hutaki kuachana na mawazo haya basi jiajiri.

Nimemaliza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…