Natafuta kombinesheni Nina ekari 50 za mashamba Bora kabisa ya mahindi Rukwa

Natafuta kombinesheni Nina ekari 50 za mashamba Bora kabisa ya mahindi Rukwa

Wadau mwaka jana nililima ekari 9 tu huku rukwa nikapata Tani 21 na kulingana na Hali ya mvua ilivyokuwa na bei za mbolea nahisi ningepata zaidi mwaka huu nimeandaa ekari 50 kama Kuna mzamiaji Kwa msimu huu unaoanza novemba anitafute tuunganishe nguvu
Muhimu tu uwe mwaminifu, na usilete ujanja ujanja pale wapambanaji watakapoanza kukutafuta kwa ajili ya huo uwekezaji.

Halafu uje utolee maelezo ya hizo hekari ulizolima vs hizo tani ulizovuna! Je, zina uhalisia? Au unataka kuwageuza fursa watu wenye tamaa ya mafanikio?
 
  • Kicheko
Reactions: EEX
Mimi nipeleke kwenye wale mbuzi kwenye msitu wa ajabu nikawachukue
 
Mpumbavu huyu, kwa msimu uliopita ulivyokuwa unawezaje kupata gunia 200 kwenye ekari 9?? Yaani kila ekari gunia 20?? Mpumbavu sana huyu
Huu ndio ujinga wa Matanzania! Kwani haki ya hewa ilikuwa mbaya sehemu zote? Kuna sehemu watu walivuna vizuri sana! Usimbeze hugo mdau kwa Rukwa na Katavi inawezekana sana!
 
TAPELI huyo. Msimu uliopita huwezi kutapa gunia 200 za mahindi kwenye ekari 9 . Kila ekari gunia 20?? Kilimo Cha wapi hiki Cha mahindi
EKARI 1 inaweza kuzalisha hadi gunia 40 kutegemea na mbegu , udhibiti magugu , kuweka mbolea kwa usahihi na kwa wakati na zaidi ukizingatia msimu vema.
Acheni kuhisi mnadanganywa in everything

Kuna watu robo EKARI wanavuna gunia 6 za debe 5 sasa piga hesabu hapa

6x5 =debe 30 sasa chukua debe 30 x9 = debe 270
Yaani hapo tumepiga robo heka ziwe 9 majibu yanakuja debe 270
270÷5=Gunia 54 sasa zidisha robo heka 9x4

54x4= gunia 216

Hiyo 4 nimemaanisha tuna robo 4 kwenye EKARI 1 so ipo sawa
Kwa kifupi ardhi zimetofautiana sana mfano , ardhi ya Kigoma maeneo ya Kibondo hata uweke mbolea EKARI 1 ni ngumu ikupe gunia 15 wakati huo hizo gunia 15 kwa EKARI huko Tarime baadhi ya maeneo unawezapata hata kama hujaweka mbolea

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Uvune gunia 30 kwa heka kwa hiki kilimo cha kutegemea mvua? Hata Japan hawavuni hizo gunia 30@heka. Kama ni hivyo kila mtu si angeenda kulima mahindi? Kama unaweza kuvuna gunia 30 kwa heka, huyo muhuni si aende bank ya kilimo akakope badala ya kuleta utapeli wa kitoto hapa kutaka mshirika?
Wakati mwingine tujaribu kujifunza,nenda mwambao wa ziwa rukwa anzia kilidai hadi mtowisa ukitunza heka moja isipotoa gunia 20-30 itakuwa maajabu tatizo watu mmeshazoea kupata gunia 5 ukiambiwa habari za gunia 30 unahisi unataka kupigwa
 
Maximum ekari moja umefeli sana isipungue gunia 15 .
Nmewahi kulima robo eka nikaambulia gunia 7,watu wengi ni wabishi humu kwa sa babu hamna taarifa sahihi kuhusu kilimo.
 
Maximum ekari moja umefeli sana isipungue gunia 15 .
Nmewahi kulima robo eka nikaambulia gunia 7,watu wengi ni wabishi humu kwa sa babu hamna taarifa sahihi kuhusu kilimo.
Ivi mkuu unajua robo eka ni meter 35 kwa 17.5?
 
Back
Top Bottom