Nawasalimuni kwa jina la Mungu, naomba niwape ufafanuzi kuhusiana na Mbegu ya Mbuzi mlizo ziseama, kusema ukweli kabisa kuna watu wanao hao Boer na Savanna hapa Tz ila naomba niwape anagalizo kama kwesi unahitaji kuwekeza ktk hizo mbegu ningeliwashauri kwanza mfanye kutembelea kwanza wafugaji wa hizo mbegu halfu ndio uamue kufuga.
Nazungumza hivyo kutokana na uzoefu wangu ktk ufugaji wa mbuzi na nipo ktk mtandao wa wafugaji Mbuzi Tz, kwa hizo mbegu ningeshauri uwasiliane na Mbogo Ranches ndio pekee weney uhakika wa hizo mbegu. Shamba lao lipo Mdaula hapo, na ukiingia Instagram utawakuta utaona kila aina ya Mbegu walizo nazo na utawasiliana nao hao.
Kuhusu ugaji wa Mbuzi wa Nyama nitawashauri uanze na Galla/Isiolo wana faa sana kwa Nyama na soko letu la kawaida. mliopo Ngara fugeni Mubende ukiwa cross na Galla/Isiolo mtapata matokeo mazuri sana.
Mlioko kigoma Fuga Buha nao niwazuri sana kwa ukuwaji na kuzaa vyema wote hao huzaa mapacha mpaka 3.
Ukihitaji ufafanuzi zaidi utauliza.