Natafuta mchumba age kuanzia 40-42

Natafuta mchumba age kuanzia 40-42

Ninatafuta mchumba mkristo age 40-42 awe anafanya kazi kama mimi na mcha mungu pia.

maelezo yako ni mafupi mno kamakweli unamaanisha kuhitaji mchumba, sifa ulizozitaja hapa si sifa pekee za msingi sana kwa mume, ungetoa wasifu wa kitabia, elimu, maumbile, ikibidi kabila n.k. n.k. unaweza kuishi na mtu asieabudu dini yoyote akawa muelewa mkaishi kwa amani na furaha, kwa hiyo nadhani uwe serious toa wasifu zaidi na pia utoe na wa kwako pia ili huyo mlengwa aone kama anaweza kujitokeza kuwasiliana na wewe
 
Sio kwamba hawapo lakini you have to go an extra mile kupata mwanaume wa age hiyo ya 40 - 42

Labda ukute aliyefiwa na mke! Swali ni pale ambapo hujui kafa ni nini!! Mimi bado mdogo na wewe watafuta wazee.
 
Embu ueleze maisha yako imekuwa je miaka yote hii umekaa kimya na sasa ndio umeamua kuolewa au umeachana nae mwaka jana?
 
No matter what happened to her, kwa kawaida mwanamke mwenye umri wa miaka 40 ambaye mi namuona ni mtu mzima hawezi kuja hapa jamvini na kutafuta mchumba. From there unaweza tu kujua kwenye ujana wake alikuwa anafanya nini?
Kawaida ya wapi? Mwanamke wa miaka 40 hastahili kuolewa? Au mtu mzima hastahili kuolewa? Na kama anastahili, asitafute? What are you talking about? "...unaweza tu kujua..." Really???? OK, Alifanya nini ujana wake?
 
Aged Singles Kama kweli mko serious mnatafuta wachumba, jaribuni sites za wenzetu nje, huko mtawakuta watu wazima wengine hawajawahi kuoa au kuolewa. Hapa ni ushamba tu mtakutana nao watu wakidhani wenzao waliochelewa kuoa au kuolewa kwa sababu mbalimbali hawastahili. Nina ndg. yangu miaka 40 hana hata dalili ataoa lini, tumemlengeshea wadada hadi tumechoka tumeacha tunasubiri tutakacholetewa. Nyie vijana acheni kuongea pumba hapa mkidhani ukumbi huu mmewekewa nyie tu. Huu ukumbi ni kwa wote wanaotafuta negative comments zenu zinaonyesha jinsi ambavyo hamjastaarabika ama kuelewa kwamba kila mtu ana haki katika eneo fulani la maisha haijalishi umri.
 
Back
Top Bottom