Ndugu yangu Mende, ile kauli ya kusema Mende kaangusha kabati ni usemi tu...Na wewe kusema Love+Money=Ndoa nao ni usemi tu. Tabia ya mtu hairekebishiki kama kweli unaona huyu dada si riziki.Kwani wahehe bado wanakula mbwa?Makonde wanakula watu?...labda konokono kwani mimi nimeshawahi kula."mad fish"
what is uchaga bwana kwanini uogope kivuli chako mwenyewe?Kuna mtu mmoja pale Morogoro, karibu na Motel d'Job anapenda hela kiasi cha kutoa roho ya mtu..mimi mwenyewe kuliko mchaga...kwani hujui kuwa "money is the media of exchange"? Kwa ujumla sote tunapenda hela na si suala la wachaga peke yao.
Vigezo vya elimu vya huyu dada mie navikubali kwani nani anataka aolewe na mtu asiye na elimu, au kazi? sisi wanaume tunahitaji wake wenye elimu, wenye hela, wasomi waliostaarabika, wenye magari ingawa hatuna ubavu wa kuhoji wameyatoa wapi hata kama wamehongwa. Binafsi napingana na wewe "KWANI UNATUFUNDISHA WOGA"ambao madhara yake ni kutuweka kitimoto cha kuonekana hatujiamini, NAMAANISHA SISI WANAUME TUTADHARAULIWA.
Usione natetea sana hoja ya huyu dada kwani hata anyway...SIMFAHAMU, SIMJUI, SIJAWAHI MWONA ILA NIMEHESHIMU SANA POST YAKE...kwanza mbona hivyo vigezo vichache sana.
Yeye alichotaka ni elimu tu ya Diploma, kwa maelezo yake hapo juu ana Shahada ya Kwanza, hata kama hajasema amejidhatiti kwenye fani gani... hivyo anahitaji mwanaume mwenye elimu . Pili mtu aliye na kazi.."kazi ni kazi" hakutaja aina ya kazi, Awe hajaoa hata kama ana mtoto sawa tu (ona anavyojali hata mtoto wa mwenzake) Awe mkristo, asiwe mvutaji sigara,...mi nadhani hata na pombe asiwe anakunywa...eti dada yangu awe mnywa pombe?..jibu tu utuondolee mashaka.
Kingine si shahada inayotakiwa, ni mapenzi ya kweli. Unaweza tu kuwa na stashahada, astashahada, au hata shahada yenyewe na bado ukapendwa au ukachemsha, "HIVYO JENGA MAZINGIRA YA KUJIAMINI KWANZA"
Na kwa wale mliooa "KAMA MIMI" tuwe wawazi inapokuwa ni suala la kumshauri mtu kama huyu badala ya kumponda jukwaani..hili ni jukwaa la heshima, lina watu wa rika mbalimbali, elimu mbalimbali, kazi mbalimbali,humu ndani pia kuna watu wenye matatizo yao mbalimbali wanahitaji ufumbuzi na WAMETUAMINI WANA JAMII kuwa tunaweza kuwashauri vyema, hivyo tusiwavunje moyo kwa kuwatukana au kuwabeza...tuwashauri tu mungu atatulipa siku moja.
Mwisho narudia ule usemi wangu kuwa NAWAKUBALI WANAJAMII WOTE , ILA NINACHOCHUJA HAPA NI HAYA MAWAZO TOFAUTI TOFAUTI TULIYO NAYO NA TUNAYOYATOA.