Mimi niweke wazi ninafanyakazi ambayo siwezi kuhama na ni ya kudumu.Hivyo mke wangu lazima awe tayari kunifuata.Mke wangu wa zamani aliingia kwenye matatizo baada ya kuwa anaishi mbali na mimi kisa kazi.Jamani hizi kazi zinazotenganisha wenzi zinachangia sana kuzivunja ndoa badala ya kuziimarisha!!Umeniuliza mke atoke mkoa gani,ni ngumu kubashiri.Mimi sioi mkoa ila mtu.Anaweza akawa wa asili ya arusha,Mwanza,Kigoma,Tabora,au Zanzibar lakini ukamkuta anaishi Mbeya kama mimi.Kwa hiyo mkoa hauna maana isipokuwa makubaliano.