Natafuta mke tutakaye-adopt watoto pamoja naye

Natafuta mke tutakaye-adopt watoto pamoja naye

Mkuu nakushauri utulie kwa Mungu, atakupa mke wa kufanana na wewe, mengine yatafuata, kama atakupa mtoto au la Mungu anajua, wazo la kuasili litafanikiwa ukimpata mke utakayepewa na Mungu, utakayefanana naye, naamini umenielewa pia nitakuombea rehema kwake maana yeye aweza yote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za leo wana JF.

Mimi ni kijana wa kiume rijali kabisa mwenye umri wa miaka 36. Nina elimu nzuri, mcha Mungu, nimeajiriwa, na nina ndoto za maisha vile vile. Kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu nimethibitishiwa na madaktari kuwa nina low sperm count kiasi ambacho siwezi kumpa mwanamke mimba.

Kwa hali hiyo basi nimebakiwa na option moja ya kuasili watoto yatima. Lakini siwezi kufanya jambo hilo peke yangu. Lazima niwe na mke. Nami sikutaka kuoa mke ambaye hata kubalina na matakwa hayo.

Nimeamua kuwa sasa ni wakati mwafaka wa kutangaza nia yangu hii kwa mwanamke ambaye pengine kwa sababu moja au nyingine naye yuko katika hali ngumu kama yangu kwamba naye hawezi kubeba mimba.

Kwa aliyetayari tafadhali niPM.

Sihitaji message zozote za maudhi ambazo hazinisaidii chochote. hujafa hujaumbika. hebu usiniongezee machungu bure wakati tayari nina machungu ya kutosha. kama haikuhusu pita kimya kimya na endelea na maisha yako. Najua kuna watu katika jukwaa hili lazima wacomment kila kitu tena kwa lugha za matusi, kejeli na kukatisha tamaa. kumbuka, kile upandacho utavuna hicho hicho. Tafadhali nyamaza.

Aliyeserious tu aje PM
Seriously I'm facing a same situation,if you still looking for ! I have a challenge of fruits of womb.asante JF.you are solution to one another ,if not today tomorrow!
 
Back
Top Bottom