UPDATE
Niseme alhamdulillah, ama hakika sifa zote njema anastahiki mola wa viumbe woote.
Kwakuwa jambo nilileta humj si vibaya pia kuleta mrejesho humu, kuna ndugu/washikaji kadhaa walikuwa wanaulizia mrejesho akiwemo bwana
Darmian na wengine wengi.
Wazee ndugu yenu nimefanikiwa, japo kazi haikuwa rahisi saana, maana waliojitokeza ni wengi kuliko nilivyokuwa natarajia, mie nilidhani ni suala jepesi tu la kuandika hapa jf atokee mtu nione siku zisogee.. Ila walitokea wengi mnoo, wanawake saafi kabisa wenye uhitaji wa ndoa wapo wengi.. Nasikitika uwezo wangu mdogo siwezi kuoa walau wawili, kwa ghafla..
Lau kama ningekuwa na uwezo ningeoa hata wa3, sababu katika kuwapunguza punguza walibaki wachache ambao naona wanafaa kabisa, ila ilinilazimu niwaache tu, sababu niliyoelekeza hapo chini.
Nimefanikiwa kwa huyu mmoja, na mahari nimefanikiwa kupeleka MAHARI, harusi ilibidi iwe mapema kama nilivyotamani, ila kutokana na mchumba mwenyewe bado yupo darasani likizo yake ni mwezi April (ndogo) na ile kubwa ni September, nilipanga iwe April, hilo ndio lengo langu, lakini MAMA MZAZI(yangu) ameniomba nisogeze mbele sina budi kufanya mwezi huo kutokana na ratiba ya mwenzangu..
shukrani kwa wote, wale walioleta mzaha na pia walioniamin na kunipa moyo.
Pia wale warembo walionifata, imeshindikana waniwie radhi, hali ipo km nilivyoeleza, inshaallah panapo uhai naweza ongeza nitawafikiria km bado mtakuwa hamjapata stara.
Nawaombea ALLAH awafanyie wepesi nanyi mpate waume wa kufanya stara kwenu, mpate waume bora, waume wa ndoto zetu, na allah awajaalie vizazi vyenye manufaa na nyinyi duniani na kesho akhera.