Mtoa Mada,
Nakuomba utambue kua Huu ni Wakati wa Anko Magu.
Hakuna Pesa yoyote inatoka kirahisi rahisi kama akili yako inavokutuma.
Wenzio humu tumo watu kibao tunafanya biashara hizo, Tumegomboa mizigo ilokwama bandarini Mara kibao tu.
Na kwa taarifa,
Hakuna sehemu matapeli wamejaa nchi hii kama maeneo ya bandari.
Na binafsi,
Nna uzoefu sana na binafsi nlishawahi kupigwa na hao matapeli wa bandari kwa hizo gia za mizigo ilokwama.
Sasa,
Hio gia uloingia nayo humu Leo hii,
Nmeishuhudia live mara 2.
1. Ilkua mwaka 2008, akipigwa 14mil Mwanamke mmoja kutoka CONGO DRC pale mitaa ya Kurasini.
2. Nyingine, akipigwa 8mil Mkinga mmoja pale Agrey-K'koo
Leo hii ni 2018,
Zaidi ya miaka 10 ilishaopita, Wewe ndo unaieleta humu jf Leo.
Tena kwa style ile ile na maneno ya utetezi yaleyale nloskia matapeli hao wakijitetea.
Inasikitisha sana kwakweli.