1. Huku wengi wanatumia utambulisho badia, waweza kukuta kwenye familia moja kila mtu ni mwanachama kwa siri na ID bandia mwisho wa siku mkakuta mnatongozana na baba yako ama kaka zako
2.Wanaume wa kuoa ni wale unaopishana nao kila siku njiani, ni wale unaofanya nao kazi, ni wale unaosali nao, ni wale majirani zako, ni wale uliosoma nao, ni wale wanaokuja ofisini kwako ama unaowakuta ofisini kwao kwenye majukumu ya kikazi
3.Tatizo lenu hamataki kuolewa na wanaume mliowazoea kwa kuwa madhaifu yao mnaijua, kwa kuwa mnadhani hawana hela, kwa kuwa mnadhani hawana hobi za matanuzi
4. Anza sasa kuwaheshimu wanaume na kila mtu kwani yule unayemtarajia awe mchumba wako sio yeye, wachuma wa kweli wanakupeleleza kimya kimya na wakikuona jinsi unavyoishi , unavyoongea na watu, tabia za marafiki zako, unavyopenda maisha ya juu na ya hanasa wananakokimbia kimya kimya.
5. Kama wewe ni mkristu kama ulivyo sema sasa anza ibada ya kila wakati na ikiwezekana jiunge na kwaya na kule uwe na tabia tofauti kabisa maana kuna vikware vimejificha humo unaweza kuharibu faili lako kabisa.
6. Kama huo mtaa ama mkoa ulipo ulishaharibu na tabia zako zinajulikana basi hama kabisa mkoa kaaze upya na ukifika huko badili tabia maana tuna tabia ya kuwahi mwanamke mpya anayekuja bila kujali huko aliko toka alishaharibu.