Natafuta Mtoto wa kiume

Natafuta Mtoto wa kiume

Mtoto ni mtoto though tunakuwaga na matamanio yetu binafsi ila mwisho wa siku vyote tulivyonavyo nu vya Mungu mpaji wetu,kwahiyo ni yeye ndiyo mwamuzi akupaje
 
hakuna kitu kama hiyo mwenyezmungu ndo mwenye kukupangia upate wa kike au wa kiume cha msingi ni kuomba mungu tu akupe watoto wenye kheir na wewe wapate kukusaidia mbeleni unaweza pata wa kiume asikusaidie chochote na wa kike ndo akakuokoa hayo yote ni mipango ya mungu muombe mungu wako akuwezeshe kupata mtoto mwenye kheir nawewe tu
Unaweza ukawa hujui chochote kuhusu hilo pia si zambi kutokujua lakini jinsia ya mtoto mnadetermine wazazi wenyewe. Vyema kama utatumia muda wako kutafuta knowledge kuhusu hilo jambo.
 
Mwombe Mungu kwa staha utapata mtoto wa kufaa kulea usijejichanganya shetani akakupa dhahama....
 
Kuna vitu hapa tu wakuu tunachanganya, katika michango mingi ya uzi huu nilizosoma.

Shahawa(semen) ina mbegu aina mbili (X au Y) na Yai lina mbegu aina moja tu (X au X), mbegu hizo hukaa katika "pair" yaani XX kwa Yai la kike na XY kwa Mbegu za kiume. Kuna 50% ya kati ya X au Y la kiume kuchavusha X au X ya kike. Ikitoke X ya kiume ikakutana na X ya kike basi mtoto ni wa kike(XX) ama ikitokea Y ikachavusha X ya kike mtoto ni wa kiume (XY).

Na vilevile katika mbegu ya kiume, Mbegu X hustahimili misukosuko na hali tete ya mfumo wa uzazi wa mwanamke na pia mwando wako ni mdogo. Lakini Mbegu Y huenda kasi zaidi kuliko X na pia sio kakamavu, haiwezi stahimili mazingira magumu kuliko mbegu X.
kwa hiyo basi Mbegu X huweza kuka mda mrefu zaidi kuliko Y, katika hayo masaa 72 yanakisiwa, mbegu Y huweza kuishi tu kwa wastanii wa juu wa masaa 24-30 na mbegu X ndio ndio huishi kwa saa 72. Ila yai la kike(XX) huishi tu kwa masaa 24.

Kwa kutumia njia ya "Bailing Ovulation Method (BOM) au Calendar Ovulation timing (COT)" unaweza kugundua ni lini yai la kike (X au X)litakua limetolea na ovari tayari kuchavushwa na mbegu ya kiume (X au Y), mfano kwa wanawake wenye mzunguko wa siku 28, siku ambapo Yai litatolea(ovulation) hukadiriwa kua ni siku ya 14 tangu mzunguko mpya wa hedhi huanze.

Basi kwa kutumia umri wa kuishi mbegu ya kiume na ya kike kutabiri jinsia ya mtoto inawezakana.

Kujamiana siku 2 au masaa 36 kabla ya "ovulation" mtoto atakua ni jinsia ya kike (XX) kwa kua mbegu Y ya kiume itakua imeshakufa kwa masaa hayo.
Na pia kujamia siku ya "ovulation" ama saa 24 baada basi mtoto jinsia yake itakua ya kiume (XY) kwa kua mbegu Y ya kiume huenda kasi zaidi ya X hivyo basi hutangulia kufika na kuchavusha yai (X au X).

Hayo yote yanategemea sana ufuatiliaji mzuri wa karibu wa mzunguko wa hedhi kwa wanawake na pia hali nziru(alkali) ndani ya njia ya uzazi kwa mwanamke.

NB: Idadi ya Mbegu X au Y huathiri matokeo hayo, kwa hiyo ifahamike huwiano sahihi na idadi sahihi ya mbegu za kiume utaboresha matokeo haya.
 
Kama mkeo mzunguko wake ni siku 28 basi hesabu kuanzia siku anayopata hedhi mpaka siku ya 14 mbandue siku hiyo hiyo na kama mzunguko wake ni siku 22 basi mbandue siku ya 12.....kila lakheri katika kazi ya kufyatua
 
Kama mzunguko wa mke wako ni cku 28 bac hesabu kuanzia cku anayopata hedh mpk cku ya 14,15,16 zte hzo ni cku ya kupata mtt wa kiume,cku ya 11,12,13 ni cku ya mtt wa kike,tafta dokta akuelekeze
 
Umeeleza kinyume..linalokaaa muda mrefu ni la kike.....
 
Back
Top Bottom