Kuna vitu hapa tu wakuu tunachanganya, katika michango mingi ya uzi huu nilizosoma.
Shahawa(semen) ina mbegu aina mbili (X au Y) na Yai lina mbegu aina moja tu (X au X), mbegu hizo hukaa katika "pair" yaani XX kwa Yai la kike na XY kwa Mbegu za kiume. Kuna 50% ya kati ya X au Y la kiume kuchavusha X au X ya kike. Ikitoke X ya kiume ikakutana na X ya kike basi mtoto ni wa kike(XX) ama ikitokea Y ikachavusha X ya kike mtoto ni wa kiume (XY).
Na vilevile katika mbegu ya kiume, Mbegu X hustahimili misukosuko na hali tete ya mfumo wa uzazi wa mwanamke na pia mwando wako ni mdogo. Lakini Mbegu Y huenda kasi zaidi kuliko X na pia sio kakamavu, haiwezi stahimili mazingira magumu kuliko mbegu X.
kwa hiyo basi Mbegu X huweza kuka mda mrefu zaidi kuliko Y, katika hayo masaa 72 yanakisiwa, mbegu Y huweza kuishi tu kwa wastanii wa juu wa masaa 24-30 na mbegu X ndio ndio huishi kwa saa 72. Ila yai la kike(XX) huishi tu kwa masaa 24.
Kwa kutumia njia ya "Bailing Ovulation Method (BOM) au Calendar Ovulation timing (COT)" unaweza kugundua ni lini yai la kike (X au X)litakua limetolea na ovari tayari kuchavushwa na mbegu ya kiume (X au Y), mfano kwa wanawake wenye mzunguko wa siku 28, siku ambapo Yai litatolea(ovulation) hukadiriwa kua ni siku ya 14 tangu mzunguko mpya wa hedhi huanze.
Basi kwa kutumia umri wa kuishi mbegu ya kiume na ya kike kutabiri jinsia ya mtoto inawezakana.
Kujamiana siku 2 au masaa 36 kabla ya "ovulation" mtoto atakua ni jinsia ya kike (XX) kwa kua mbegu Y ya kiume itakua imeshakufa kwa masaa hayo.
Na pia kujamia siku ya "ovulation" ama saa 24 baada basi mtoto jinsia yake itakua ya kiume (XY) kwa kua mbegu Y ya kiume huenda kasi zaidi ya X hivyo basi hutangulia kufika na kuchavusha yai (X au X).
Hayo yote yanategemea sana ufuatiliaji mzuri wa karibu wa mzunguko wa hedhi kwa wanawake na pia hali nziru(alkali) ndani ya njia ya uzazi kwa mwanamke.
NB: Idadi ya Mbegu X au Y huathiri matokeo hayo, kwa hiyo ifahamike huwiano sahihi na idadi sahihi ya mbegu za kiume utaboresha matokeo haya.