Natafuta Mtu anayeweza kunikopesha kwa kuweka dhamana ya camera

..futa namba za ndugu zako wote bakiza za wazazi wako kama wote kwa ujumla hawana elf 70 hadi uje uombe huku wanafaida gani?
Ukiona hivyo kasuswa na ndugu na marafiki kwa mkorofi wake wa kutorudisha pesa akikopesha ndio hupata hiyo shida

Unamkopesha elfu mbili kurudisha anajifanya kasahau wewe uliyemkopesha ndio uhangaike kumfuatilia

Na ukimfuatilia mkali yaani elfu mbili tu ndio unanidai hivi.Elfu mbili nayo hela nitakupa siku ingine hakupi!! Sasa siku ingine akihitaji hela ya kukopa hata elfu moja tu anazunguka kwa ndugu na marafiki wote hapati hata kama matajiri wenye pesa za kutosha hawatoi hiyo elfu moja.Ndio hawa kama huyu wanakuja kulia lia jamiiforums humu

Abiria Chunga mzigo wako
 
Duh, umenistua ila ngoja tu nimcheki kama vipi nimpe tu hiyo 50...huenda ana ishu muhimu ya kusolve.
 
Aah kumbe😁
 
Mimi nikikutana na Mtu na kuongea nae ndio najua kama yupo real au anadanganya, ngoja nikutane nae kwanza nijue.
 
Mimi akinithibitishia kuwa hiyo kamera kweli ni ya kwake kwa vielelezo vya risiti naweza kumpa hiyo pesa tena tunaandikishiana sio anipe kienyeji tu baadae iniletee kesi.
 
tapeli na mgumu kulipa madeni ya watu hilo kamera isije kuwa ulitapeli au wizi jumba bovu likamwangukia anayekukopesha
Hapa ndio kwenye mteego hiyo Camera nadhani haipungui 500+K kama ni used kibongobongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…