Ngoja nikuambie: maelezo yako yanajitosheleza kabisa. Kila kitu kiko clear. Kama kuna mtu ana nia ya kuwekeza basi ataku-contact na mtapeana details zaidi. Hapa JF mimi ni mkongwe na nikutahadharishe. Asilimia kubwa ya wanaouliza maswali na kukulaumu kwa nini hujibu ni wa kupuuza/kuwaambia watumie PM kwani either hawana nia au uwezo wa kuwekeza. Kingine: Utafuatwa sana na matapeli na pia wanaume ambao wanataka kutumia hitaji lako kwa manufaa yao, hivyo uwe mwangalifu sana. Kuna dada mmoja yamemkumta. Alitaka kufanya biashara ya ubia kama wewe akatangaza, akatokea jamaa mmoja akamwambia ana nia ya kuwekeza. Wakapanga kwenda sehemu kupeana details, jamaa akanunulia soda wanywe wakati wanaongea. Matokeo yake dada akaleweshwa na madawa na kuporwa kila kitu. Nasema tena: uwe mwangalifu sana na hata kama kuongea nendeni sehemu unazojua wewe ni salama na kila mtu mchukulie kwa tahadhari.