Natafuta mtu wa kuwekeza mtaji kwenye biashara ya utalii

BLUE BALAA

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2010
Posts
1,222
Reaction score
776
Mimi ni mfanya biashara wa mambo ya utalii katika malazi na ushauri wa biashara katika mambo yanayo husiana na uwekezaji katika biashara ya utalii. Nina uzoefu mkubwa katika biashara hii na ni msomi wa ngazi ya stashahada na shahada ya utalii na utawala wa biashara. Nimeyumba katika biashara kuanzia mwaka 2016 ambapo nililazimika kufunga hoteli yangu Karatu na baada ya hapo baada ya Covid nilifunga lodge Serengeti. Kwasasa biashara ina anza kufunguka na kuanzia mwezi wa sita mwaka huu kutakuwa na bishara. Mpaka sasa matarajio yangu ya biashara mpaka mwezi wa kumi na mbili 2022 nategemea kuwa na mauzo ya dola za kimarekani 162,000 sawa na Tshs 385,560,000. Nikiwekeza ngungu zaidi kwa masoko naweza kwenda mbali zaidi.

Katika kipindi hiki cha takribani miaka nane kampuni yangu imeyumba mno katika mzunguko wa fedha kiasi kwamba tunashindwa kufungua tena biashara zetu na ndio maana natafuta kampuni itakayoweka kiasi cha fedha kwa ajili ya mtaji wa kufanyia kazi ambapo tutatoa faidi zaidi ya bank na pia atahusika moja kwa moja katika uendeshaji ili kuangalia maslahi yake.

Niko tayari kukaa na yeyote chini kujadili namna bora ya kufanya biashara hii. Naomba alieyeko serious anijie inbox tupange.

NAWAKILISHA
 
Kwa rasilimali ulizo nazo na mpango wako mzuri wa biashara, haina shaka ukienda benki utapewa pesa unayoitaka. Kwa nini hujaenda?

Kwa sababu ya uviko biashara ya utalii bado ni risky. Kwa hiyo watu wenye pesa zao wanaogopa kuwekeza huko.

Sababu nyingine ni ile hali iliyopo kwamba kila mtanzania anataka awe yeye ndiye mwenye biashara aka private ownership. Desturi ya kufanya biashara moja na shareholders zaidi ya mmoja ni kama inatunyima uhuru wa kutumia pesa yangu
 
Risky ya utalii unayoingolea wewe bank pia wanaiona hayo mengine ya shareholder wengine mimi siko huko kwani my partner is my wife ambao we are all sailing on the same boat
 
Sio Kweli ?

Kipindi hiki cha urefu wa kamba zao kuna watu wana pesa chafu ya kusafisha hawajui waifanyie nini na kwao ummiliki wa asset ni prestige its all about Salesmanship ya huyo mdau kama anaweza kupiga sound na ana personal skills atafanikiwa....
Inawezekana akabahatisha, ingawa inaweza kuchukua muda mrefu, kwa sababu sisi waafrika kuaminiana kwenye uwekezaji wa partnership ni tatizo.
 
Kweli kabisa wala mimi simshauri sana partnership hata mkikubaliana mwisho wa siku ni matatizo ugomvi wa kila siku na mwisho wa siku mnaishia kupigana..., Point yangu ilikuwa kwenye watu wenye pesa chafu za ma-deals (ambao kwa sasa wapo) hao wakiona kuna opportunity ya kusafisha pesa zao hapo anaweza kwenda nao kidogo kidogo....

Kuanza kwenda Benki sasa hivi na kupigwa ma-interests ya kufa mtu ni risky unaweza kuruka majivu ukaingia kwenye moto...

Vilevile huenda hapo akawa anauza zaidi skills zake kuliko hata assests alizonazo..., hence kwa ushauri kama ana uwezo wa kupata customers aingie maelewano na wafanyabiashara wengine (same industry) ili wateja wake wakija for next few seasons atumie facilities za hao wenzake (kwenye same industry)
 
Inahitajika kiasi gani?cha pesa kuwekeza.
Hili naliona nijema ndio maana MAMA anapambana mnooo kubusti tena na pesa itapatikana tu na mafaida lukuki
 
nipe share kama asilimia 30 kwenye kampuni yako otherwise BIG NO
 
Inahitajika kiasi gani?cha pesa kuwekeza.
Hili naliona nijema ndio maana MAMA anapambana mnooo kubusti tena na pesa itapatikana tu na mafaida lukuki
Kwamba amepata a Magic Bullet ?

Nadhani wadau kama huyu ndio wanaoboresha Utalii kuliko mtu yoyote, wapo field na wana-experience hayo mengine ni more politically the only thing government can do ni Sera bora kuwawezesha hawa jamaa au uwekezaji on the field (sio kuwakamua kwa makodi yasiyo ni kikomo)
 
Tatizo mkianguka hamtaki kukubali ,eti niweke hela yangu afu ukisimama uniteme maana website yako hotel zako kampuni zako ,weka share mezani tukupe kibunda

Nasisitiza wafanya biashara wengi bado wana ili tatizo. Biashara kama inakulipa na mtaji ni shida kwa nini usiongeze sheha au ukauza sheha kwa watu ukakuza mtaji dse ipo pia. Wanataka wapewe hela vitu vikinyooka faida yako inakatiwa hapo hapo.
 
Back
Top Bottom