Nimepitia, comment zote lakini sijaon hata mtu mmoja ambae ameonyesha nia ya au hitahji la huyo dada, kisa aamesema ana HIV. lakini kumbukeni hao mnaokutana nao kila siku hawajawaambia status yao. Ila mnakula mpaka chumvi.
Pia Njia za kupata ukimwi zipo nyingi mfano
- Kuwekewa damu yenye virusi,
- Kuzaliwa na mama mwenye virusi (PMTCT)
- Kushea vitu vitu vyenye ncha kali na mtu mwenye virusi
- Kwa njia Ngono ( Popular means of transmissions).
Hata hivyo mtu mwenye maambukizi ya HIV hazuiliwi kuoa au kuolewa, isipokuwa ni muhimu kuonana na mtaalam
kabla hajapata ujauzito ili amshauri.
Lakini mtu huyu anaweza kuolewa na kuzaa na atafuata masharti kuna uewzekano mkubwa mtoto aliyepo tumboni asipate maambukizi. Tafiti zimeonyesha wamama wanaotumia dawa za ART wakati wa ujauzito wana 95% ya kutoambukiza watoto wao.