Natafuta mume

Natafuta mume

Status
Not open for further replies.
ushawahi kuona mjamzito wa miezi 6 anataka agongwe na gari sababu ya aliyempa ujauzito na yeye anachekelea?Nimenusurika kufa,nimedhihakiwa,nimetukanwa,nimepigwa nimepoteza mali mwanangu kapewa roho ya kukataliwa hata kabla hajaja duniani naimani mpaka sasa nipo hai ni kwa sababu ya bguvu ya Muumba aliyejuu
Umesema ulikua unasoma humu kwa muda mrefu natumaini ulikua unaona majibu mabovu hivyo ulijiandaa kwa hilo.

Maneno ya humu yasikushughulishe, fuata kilichokuleta.

Na itakua kama unavyotaka.
 
h
Alikutelekeza......Je moyoni mwako bado yupo?... na hata akirudi sasa hivi mnaweza kuyaanzisha upya?.....!

Kuna kitu Wanawake wengi sana mnakosea, nacho ni kuzaa na mwanaume ambaye hajakuoa, hilo ni kosa kubwa sana. Mnajiaribia maisha yenu wenyewe kwa matendo yenu ya tamaa.

Anyways, kila la kheri katika kutafuta Mume, nisiandike mengi nikawakatisha watu wengine tamaa.
hayuko moyoni nikiri tu nimekosea ila naomba nsinyanyapaliwe
 
ushawahi kuona mjamzito wa miezi 6 anataka agongwe na gari sababu ya aliyempa ujauzito na yeye anachekelea?Nimenusurika kufa,nimedhihakiwa,nimetukanwa,nimepigwa nimepoteza mali mwanangu kapewa roho ya kukataliwa hata kabla hajaja duniani naimani mpaka sasa nipo hai ni kwa sababu ya bguvu ya Muumba aliyejuu
Siku zote majuto ni mjukuu, wewe ukiwa kama msomi chuo, you should have known better! Haya mambo ya kuchezewa na kuachwa waachieni wale wa darasa la saba. Lakini inapofika eti hata Graduate wa chuo kikuu unachezewa na kuachwa hapa ndipo huwa naona elimu yetu bado ni shida sana.
 
Mimi ni msomaji mzuri wa humu muda mrefu sana,najitokeza kwenu kutafuta mume ambae yuko tayari kwa ndoa na kupima ukimwi.
Wasifu.
Ni mama wa mtoto mmoja.
Naishi Dar es salaam.
Elimu yangu chuo kikuu japo kwa sasa sina ajira.
Umri wangu miaka 30.
Mkristo.
Mwanaume nimtafutae.
Kuanzia miaka 32.
Awe anajitambua na ajue nini maana ya mke na familia na amkubali na kumpenda mwanangu kama mwanae wa kumzaa
Awe tayari kupima ukimwi.
Nahitaji mwanaume aliekuwa serious muda wa kupotezeana sina asiwe na mahusiano yoyote anipende sana na kunilea kama yai maana mie najua kupenda sana na ninajua nini maana ya mwanaume.
Karibuni
Once again , umri
 
Siku zote majuto ni mjukuu, wewe ukiwa kama msomi chuo, you should have known better! Haya mambo ya kuchezewa na kuachwa waachieni wale wa darasa la saba. Lakini inapofika eti hata Graduate wa chuo kikuu unachezewa na kuachwa hapa ndipo huwa naona elimu yetu bado ni shida sana.
ahsante
 
Mkuu miminimama siku zote mimi huwa napenda kuwaambia watu ukweli wao ili wale wengine wasije wakarudia makosa yale yale. Sina ubaya na wewe na wala sina chuki na wewe. Mimi nimejipa jukumu la kukemea maovu humu JF.

Haina maana kwamba hutapata Mume, hapana, Mume utampata lakini inabidi uwe makini sana mara hii maana unaweza ukajikuta unabebeshwa Mimba nyingine na kuachwa tena. Why?... sababu sasa hivi uko lonely and desperate, unatafuta mume kwa bidii, some men can take advantage of that situation na kujifanya wanakupenda sana na kukujali, kumbe lengo lao ni kukuchezea tu huku wakiwa hawana nia ya future na wewe. Utakapopata ujauzito tu usishangae akakimbia tena kama yule wa mwanzo.

Kuwa mwangalifu sana tena sana.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom