Natafuta muwekezaji

Natafuta muwekezaji

Ofsa Kidali

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2021
Posts
212
Reaction score
119
Habari za muda huu wana JF, hongereni kwa mapambano ya kila siku kuifanya dunia kuwa bora na salama.

Mimi ni kijana wa kitanzania mkazi wa Dar es Salaam elimu yangu ni kidato cha sita. Awali kabisa napenda ieleweke kwamba dhumuni ni kukuza na kuiboresha biashara (sitasema biashara yenyewe hapa kwa sababu za kimaslahi) kwa maana kwamba biashara tayari ipo(Gongo la mboto, Dar es Salaam). Kiasi kinachotakiwa hapa ni Tsh.3,500,000/=(Milioni tatu na nusu).

Kinachokwenda kufanyika ni kuizalisha pesa yako kufikia mara mbili ya kiasi unachowekeza katika kipindi ambacho kitakuwa ni cha ahueni kwa pande zote mbili (biashara na muwekezaji) na kipindi chenyewe kitaamuliwa baada ya mazungumzo kati yetu. Tafadhali jongea PM kwa maelezo na mazungumzo zaidi ikiwa una nia ya dhati. Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu.

•Kwa kudokeza tu, biashara imejikita katika utoaji huduma.

•Makabidhiano ya pesa yataambatana na utiaji saini kwenye mkataba chini ya usimamizu wa serikali wakiwemo mashahidi wa pande zote mbili.

•Mkataba wetu utakuwa umekoma baada ya pesa uliyowekeza kufikia mara mbili.

•Napenda kukushauri kufika kujionea biashara yenyewe kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho kwasababu ni biashara ambayo imejipambanua kipekee kwa hiyo itafaa sana upate picha kubwa"THE BIG PICTURE."
 
Sales zako ni kiasi gani kwa siku tuanze hapo na kwa hesabu zako iyo pesa ita double baada ya muda gani
1.Sales(mauzo) ni Tsh.35,000/= kwa siku na bado nazidiwa na uhitaji wa huduma kwa maana kwamba biashara ikitanuka itaweza kukidhi wateja na hivyo basi kupelekea mauzo kupanda.
2.Suala la pesa itadouble lini si rahisi kama utalitafakari kwa kina na hivyo basi hakuna budi kwa pande zote mbili(biashara na muwekezaji) kujadiliana na kuja na hitimisho la muda ambao utakuwa ni wa ahueni kwa pande zote mbili kama nilivoainisha kwenye uzi.
Kongole kwa maswali mazuri mkuu.
 
Ok so ni bishara ambayo tayari inatembea....hii inanikumbusha kipindi cha dragons den. Hiyo hela unahitaji kwa mkupuo?
 
Nilwahi kuwa na swahiba wangu ambae alikuwa akifuatilia sana Dragons den BBC.
Ndio, hela inahitajika kwa mkupuo.
 
Fatilia hizi comments mtu anayekuja kucomment coment ya 19 mng’ang’anie anayo pesa na yupo radhi kuwekeza.. nakusisitiza usimuache mkuu akikoment tu mfate inbox moja kwa moja.. akikoment vyovyote vilee muendee inbox
 
[emoji2][emoji2]
 
Aisee! 😳😳
 
Habari za muda huu wana JF, hongereni kwa mapambano ya kila siku kuifanya dunia kuwa bora na salama.

Mimi ni kijana wa kitanzania mkazi wa Dar es Salaam elimu yangu ni kidato cha sita. Awali kabisa napenda ieleweke kwamba dhumuni ni kukuza na kuiboresha biashara (sitasema biashara yenyewe hapa kwa sababu za kimaslahi) kwa maana kwamba biashara tayari ipo(Gongo la mboto, Dar es Salaam). Kiasi kinachotakiwa hapa ni Tsh.3,500,000/=(Milioni tatu na nusu).

Kinachokwenda kufanyika ni kuizalisha pesa yako kufikia mara mbili ya kiasi unachowekeza katika kipindi ambacho kitakuwa ni cha ahueni kwa pande zote mbili (biashara na muwekezaji) na kipindi chenyewe kitaamuliwa baada ya mazungumzo kati yetu. Tafadhali jongea PM kwa maelezo na mazungumzo zaidi ikiwa una nia ya dhati. Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu.

•Kwa kudokeza tu, biashara imejikita katika utoaji huduma.

•Makabidhiano ya pesa yataambatana na utiaji saini kwenye mkataba chini ya usimamizu wa serikali wakiwemo mashahidi wa pande zote mbili.

•Mkataba wetu utakuwa umekoma baada ya pesa uliyowekeza kufikia mara mbili.

•Napenda kukushauri kufika kujionea biashara yenyewe kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho kwasababu ni biashara ambayo imejipambanua kipekee kwa hiyo itafaa sana upate picha kubwa"THE BIG PICTURE."
Mkuu unatafuta muwekezaji JE,Muwekezaji atakuwa MMILIKI?Atamiliki percent ngapi?Je kama sio mmiliki utakuwa ni mkopo?Mkopo wa muda gani na masharti gani?Kusema tu ela itakuwa mara mbili haitoshi.Kuhusu mikatabansio tatizo tatizo ni masharti ya huo mkataba.

Mimi naweza kukupatia kiasi hicho cha PESA kwa makataba wa Mwezi mmoja dhamana iwe asset kama vile gari au kiwanja au nyumba na nitahitaji faida ya 10% kwa mwezi sio zaidi.Vipi Utayaweza hayo masharti?
 
Back
Top Bottom