Natafuta mwalimu wa martial art

Foxhunters

Senior Member
Joined
Nov 25, 2019
Posts
160
Reaction score
108
Habari, wakubwa mimi kijana wa kiume 31 miaka.

Naomba kwa mtu anayeweza kuwa mwalimu wangu wa ngumi, au kuniunganisha na mwalimu wa martial art, awe anapatikana manispaa ya kigoma ujiji.

Nilikuwa na ndoto hii kwa muda mrefu ila sikuweza kuitimiza ijapokuwa umri umeenda niko tayari kujifunza . Muda wangu ni kuanzia saa tisa na nusu jioni mpaka usiku na weekend.

Niko tayari kujifunza kwa nidhamu ya hali ya juu sana.
 
Mtafute Sensei adriz au Sensei Bujibuji Simba Nyamaume au Sensei King Kong III utajua kuliko hata Bruce Lee sawa?
 
Anza na muuza madafu...
 
Umri umeshaenda huo na hautaona faida wala manufaa ya huo mchezo, 😂😂😂
 
Tujue kwanza dhumuni lako la mafunzo haya unayoyataka ni kwa minajili gani baada ya hapo tutajua namna ya kukusaidia
 
Saa tisa siyo jioni Bali alasiri/Al asr
 
Siku hizi ngumu ni ghafla tu,wakosa adabu wengi
Ni kitu nilikuwa napenda toka utotoni sema malezi yalinibana sana, zikaba harakati za shule nako nikawa nimebanwa na mazingira. Na hata nulipo ajiliwa kwa mara ya kwanza nikapelekwa vijijini,Sasa ni baba najitegemea na wakati sahihi kwangu kutimiza ndoto yangu.
Pia,wanangu nataka waanze wakiwa na umri mdogo .kwa Sasa wana umri wa miaka 4 na mwingine 1.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…