Natafuta Mwanamama wa kushirikiana nae kwenye biashara ya Chakula (Mama Ntilie)

hbi

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2011
Posts
678
Reaction score
298
Habari wanajamvi, ninatafuta mtu wa kushirikiana nae kwenye biashara ya kuuza chakula maarufu kama Mama Lishe. Ninapendelea huyo mtu awe na uzoefu wa biashara hiyo kwani atakuwa mpishi mkuu.Pia awe anaishi Dar es salaam, Tutazungumza makubaliano yatakvyokuwa ila kwa ufupi mimi nitatoa gharama zote zinazotakiwa za kuanzisha biashara hii. Tutaelewana namna ambavyo tutagawana nae faida itakayokuwa inapatikana. Ambaye yupo tayari au kama una mtu unamfahamu anaweza mwambie awasiliane na mimi kupitia simu namba 0678692973. Tuma meseji tafadhali.
 
Kuna member miyeyusho kishenzi. Sasa mtu anaulizia deals za biashara wewe unamletea maswala ya ngono.
Au unataka upunguze ushindani uende wewe?
 
Unatafuta mtu wa kushirikiana naye au unatangaza kazi kuwa unahitaji mpishi mkuu? Eleza mshahara sh ngapi watu waombe kazi. Hakuna ushirikiano ambao mtu mmoja anatoa kila kitu zaidi hapo naona unataka kumnyonya mtu kaa kisingizio cha ushirikiano.
 
Maelezo yamejitosheleza, kama unaona hakuna ushirikiano wa namna hiyo Sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…