Natafuta mwanaume H.I.V Positive mrejesho

Natafuta mwanaume H.I.V Positive mrejesho

akadunda nini? teh teh nimecheka sans
[emoji23][emoji23][emoji23]
Wanaishingi miaka zaidi ya hiyo rafiki..
Nilishawahi kuwa na girl friend baba yake alikufa na UKIMWI akiwa darasa LA tatu Leo huyo Dada kamaliza chuo kikuu na yuko kazini mwaka Wa tano lakini mama yake yupo hai.
 
Wanaishingi miaka zaidi ya hiyo rafiki..
Nilishawahi kuwa na girl friend baba yake alikufa na UKIMWI akiwa darasa LA tatu Leo huyo Dada kamaliza chuo kikuu na yuko kazini mwaka Wa tano lakini mama yake yupo hai.
oa huyo man hao ndo tunasikiaga kwenye tv mke mwema
 
yes...mimi ni mfano hai...my viro load are undetected..kiasi kwamba nilipima juzi kazi dispensary wakaniambia sina virusi...nikachukua majibu huku nacheka...nadhani na kipimo chao kilikua kibovu..ndio maana wanasema test 3 times...if nimeenda na mtu si anajua niko okay...complicated
Lakini antigents huonekana
 
thebeliever

Baada ya miezi sita hivi ya jaribio la kupata mwenza umtakaye, umefanikisha nia yako?

Kama hujafanikiwa, utatumia njia hii kuendelea na zoezi la kupata mwenza ama utabadili mbinu?

Nikutakie kila la kheri
 
Mtu kama mimi nayependa kupiga mbichi unanishauri ni dada yangu?mwaka wa 20 huu mm napiga kavu tu
acha kejeli ngoma yaweza kumpata yeyote yule uwe unagonga au hugongi ....usijione upo bora zaidi na kuona kamwe ukimwi wameumbiwa wengine na wewe kamwe haitokaa itokeee kuupata ...ndugu kuwa makini na maneno yko

narudia tena acha kejeli ukimwi unaweza kumpata yeyote yule OMBA MUNGU TU AKUEPUSHIE NA JANGA KAMA HILO
 
Binafsi sitaki kukupa pole sababu wewe ni mwanamke jasiri sana, pia unayethamini wengine. Kwa roho hiyo na ujasiri ulionao naamini MUNGU ni muweza wa yote na ugonjwa wako unaenda kupona na utaleta mrejesho hapa hapa JF kuwa umepona.
MUNGU akutangulie na akupe nguvu.
 
Inatokea sana
Kuna mama alifanya makusudi kumtuma boyfriend wake kutembea na mtoto wake wa kambo mpk akampa mimba na kumuambukiza

Huyo mtoto wa Kambo kwani alibakwa? Si alipigwa mashine akijua anatembea na mchepuko wa mama wa kambo? Inabidi tuwe responsible kwa maamuzi yetu tusiwasingizie wengine.
 
Hi guys ni matumaini yangu mko poa

Nimerudi tena hapa love connect,nataka kushare na wengi au wachache wenye kupenda maisha ya wengine

Kwa kipindi chote tokea nitoe tangazo hapa.Nimekuwa nikipata connection za watu wengi ambao wako -ve na ambao wako +ve

Nashukuru Mungu nimeweza kujisimamia,na kusimamia.Kuna wanaume walikuja kwa njia mbali mbali nili deal nao kwa namna ya wanavyokuja,wengine tuliishia kuchat tu maana aliekua anania alikua na subira na nilichukua takribani miezi 3 mpaka kuja kuonana

Wengi waliishia njiani,nilifanikiwa kupata wanaume 4 walio serious kwa dhamira zao lakini wawili walikua wana influence ya familia hawataki mkristo na mmoja hatukufanikisha wazazi wake walihitaji mwanamke wa kabila yake mmoja alisisitiza kuishi bila kuzaa maana alikua na watoto wawili.

Nilifanikiwa kupata wanaume 3 ambao walikuwa -ve na walikua tayari tuishi nilidhani ni uwongo na kujihakikishia tulienda kupima na nilijiridhisha walikua salama lakini kama awali nilitangulia nisingependa mtu aje kulia kwa ajili yangu hata kama aliamua yeye hivyo sikuwa na sababu ya kuendeleza mahusiano.

Pia nilipata wanaume 2 hawa walikua +ve ila hawakua tayari kushiriki mapenzi safe ili kutozalisha maambukizi mapya hivyo pia ilibidi tuishie tulipoishia nilichogundua watu wengi wanatatizo na watu wengi wamekata tamaa wengi wanasambaza virusi kwa makusudi inahitaji akili sana kupambanua mambo.

Kwangu mimi nimejifunza mengi maana nimejionea mengi lakini bado nadhani ninasafari ndefu ya kukamilisha ndoto zangu so nahitaji mtu wa kunyanyuka nae katika hali zote.

Kwa wale wenye tatizo kama yangu jitahidi kufanya selection at least upate mtu ambae anauelewa kuhusu VVU na awe na future bila kuangalia hayo unaweza kuishia kupata mambukizi mampya na lifetime stress wengi wetu tunakufa kwa stess na sio kirusi so watch out

Na wale mlio salama nawakumbusha play safe unaweza kuwa positive muda wowote onyesha upendo kwa victims muombe mungu sana

Mimi sikuzaliwa na ukimwi niliambukizwa na mama wa kambo kwa makusudi lakini nimesamehe na maisha yanaendelea na sihitaji kumuambukiza yeyote.

Asanteni
inauma sana!
 
Kama nakujua vile, mama yako wa kambo (shombe sijui wa kijerumani) aliyekuambukiza alifariki mwaka jana, alikuambukiza kwa kukuuma na meno yake mkiwa mnapigana, baba akaoa mke mwingine mwaka jana huo huo, mama mpya ni kabinti kadogo kama wewe, na sasa wana katoto kadogo ka kike, baba hakuzaa na mama wa kambo, uliwahi kupata mchumba aliyekubali kukuoa japo yeye hajaambukizwa ila mama wa kambo alifanya figisu uchumba ukaisha, sasa hivi una mgogoro na baba kwa kuwa umehama kanisa katoliki
 
Kama nakujua vile, mama yako wa kambo (shombe sijui wa kijerumani) aliyekuambukiza alifariki mwaka jana, alikuambukiza kwa kukuuma na meno yake mkiwa mnapigana, baba akaoa mke mwingine mwaka jana huo huo, mama mpya ni kabinti kadogo kama wewe, na sasa wana katoto kadogo ka kike, baba hakuzaa na mama wa kambo, uliwahi kupata mchumba aliyekubali kukuoa japo yeye hajaambukizwa ila mama wa kambo alifanya figisu uchumba ukaisha, sasa hivi una mgogoro na baba kwa kuwa umehama kanisa katoliki
hapana...
 
Back
Top Bottom