Huwezi kwenda kwenye hatua ya mume na mke bila kupitia urafiki, upenzi, uchumba n. k au samahani mume ni nani anapatikana vipi
Nikwambie kitu ndg yangu. Mila zile za kale za mababu, zilikuwa na maana njema kabisa.
Nasi tukizifuata,kuziheshimu na kuzitumia, zinaweza zikatusaidia pakubwa.
Kutafuta mchumba wa kuoa ni tofauti sana na kutafuta rafiki ama hawara.
Uthamani wa mwanamke ni uke na umwanamke wake. Thamani hizo hazitakiwi kuguswa ama kuchezewa hovyohovyo na kila mtu. Pia, heshima na staha kwa mwanamke, ndiyo viongeza thamani yake. Kinyume cha hayo ni mwendo wa unungayembe.
Kwenye kuoa hakunaga sura ama ulimbwende. Mwanamke mzuri ni tabia yake mwenyewe.
Wachumba hawakuruhusiwa kukaribiana kabla ya ndoa. Hiyo ilikuwa na maana njema, wachumba iliwapa moyo na juhudi za kufuatiliana ili waoane, mtu alijinyima hata kula, apate pesa ya mahari,aweze kummiliki haraka mchumbaake,kwa kuwa ana "muhu" nae, hajawahi kumgusa hata siku1! Lkn fikiria kama kitu ushawahi kukitumia, utakuwa na pressure kukipata? Tena hata ikashindikana, hakuna hasara. Itabakia aibu kwa wazazi.
Hili la kuanza na uhawara, urafiki, cjui kupiga uhuni, kufikia hatua ya kuoana huwa ni suala la kubahatisha. Masuala ya kuunganisha watu hadi kufikia kuoana ni mambo ya kisaikolojia. Na kanuni nilizozieleza hapo juu zinatakiwa kufuatwa.
Vinginevyo ni ndoa za mwendokasi, zenye kuhimili wiki2, kama vile wanandoa walikuwa na maagizo toka kwa mganga wa kienyeji wakafunge wakafanye harusi kwa ajili ya kuondoa mikosi.