hizi ni dalili za kujikataa na kukata tamaa na hata jina lako linaonyesha kuwa umejikataa! kwa hali hii inaonyesha kuwa kwa kuwa wewe umeanza kujikataa hivyo sasa unataka ukataliwe!
hii inawezekana inatokana na mateso na masumbufu uliyoyapata huko nyuma na wanaume na mwisho wa siku unafikiri unaweza kujitawala mwenyewe.
mwanzo kwa maisha ya kawaida haisumbui lakini kwa maamuzi yako yanaweza kukutengenezea magonjwa siku zijazo ya pressure na kisukari yanayoweza kuwa yametokana na ubinafsi wako ambao unaanza kuujenga sasa!
kwa kuwa swali la mwanao baba yuko wapi litakukera na hautakuwa tayari kumpa majibu mazuri na matokeo yake utaona maumivu aliyonayo na hiyo hali itakupa shida katika maisha yako.
nakushauri yafuatayo:-
- kwanza badilisha hilo jina unalotumia kwa kuwa linaumba hali ya kukataliwa kwako na kujikataa
- pili jiamini na amini bado unafursa sawa ya kuweza kuwa na mume kama wnawake wengine
- jifanyie SWOT analysis na hakikisha unajipa maksi za juu kwanza na pale penye mapungufu hakiksha unapajazilizia kwa mazuri ulionayo
- tafuta watu wakufanyie huduma ya maombi au cancelling unaowaamini wanaweza kuwa msaada kwako na jifunue kwao (hali yako ) nao wanaweza kukusaidia kubadilika
- mwisho amini kuna mtu anakutafuta hajui atakupata lini
- kwa maelezo mengine ni pm (sio kama najipigia pande hapana nahitaji uwe mwanamke uliyefanikiwa katika mawazo yako na fikra zako ukiwa umekombolewa na utumwa wa maumivu ya ndani)