Mr Ballo
Member
- Apr 21, 2024
- 43
- 83
Habari zenu wanajamii,
Natumaini mko salama. Nimeamua tena kuweka tangazo hili kwa lengo la kukutana na mwenza wa maisha mwenye nia thabiti na malengo ya dhati.
Mimi ni mwanamume mwenye umri wa miaka 38, naishi Dar es Salaam. Natafuta mwanamke Mkristo mwenye umri wa miaka 25 hadi 35, mwenye maono ya kujenga uhusiano wa imara, wa heshima, na unaoelekea kwenye ndoa.
Itapendeza zaidi kama anaishi hapa Dar es Salaam, lakini kama yupo mkoa mwingine, ningefurahia kama anaweza kuwa na utaratibu wa kufika Dar mara kwa mara au awe tayari kuhamia hapa ili tuwe karibu zaidi.
Sina ubaguzi wa kabila, ila nikimpata mwenye asili ya Kichaga itanipendeza zaidi.
Muhimu zaidi ni mtu mwelewa, mkweli, mwenye heshima, na anayetafuta mapenzi ya dhati na maisha ya ushirikiano wa milele.
Napenda kusisitiza jambo moja muhimu sana:
Katika tangazo langu la awali, walijitokeza wanawake wachache — lakini kati yao hakuna aliyekuwa na dalili za nia ya dhati.
Wengi walionyesha dhahiri kuwa walikuja kwa nia ya urafiki wa mawasiliano tu — kupiga simu, kutumiana ujumbe, na kupotezeana muda bila kuwa na malengo makubwa au hatua za maana.
Naomba ieleweke wazi kuwa mwanamke unapopatwa na upweke wa urafiki wa kiume(Boyfriend) au umegombana na mwenza wako, suluhisho haliwezi kupatikana kwa wanaume tunaotafuta mahusiano ya kudumu, usijisahaulishe kuwa wewe wakati huo unahitaji mwanaume wa kupunguza mawazo tu au kufurahi nae kwa muda mfupi tu halafu umuache na uende kwa mwenza wako baada ya kumaliza ugomvi wenu mnarudiana.
Yaani inavunja moyo sana kwa mimi niliyekuja hapa kwa nia thabiti ya kutafuta mwenza wa maisha halafu wewe unaleta drama za kuendekeza starehe na mitoko ya anasa na kutoa taarifa za uongo eti uko msibani umekwama nauli hapo hapo mwenye nyumba anakudai kodi, eti huna hela ya kula, gafla mkataba na kampuni unayofanya kazi umeisha leo, eti kwa sasa unatafuta kazi, unasahau ulijitambulisha kuwa wewe ni mjasiriamali umejiajiri na unaishi kwa wazazi wako... kwakweli inashangaza sana na sijui kwanini wanawake wa aina hiyo bado wanaendelea kufanya hivyo vituko dunia ya leo!
Hivyo, naomba kwa heshima na unyenyekevu:
Wale wasiokuwa na nia ya dhati au wanaotaka mawasiliano ya kujifurahisha tu, tafadhali siwahitaji kabisa.
Ni vyema kila binadamu tukajifunza kuheshimu hisia za watu, hasa pale mtu anapokuja kwako kwa matumaini na imani kuwa atapata majibu ya maswali aliyonayo.
Sio busara kucheza na hisia za mtu ambaye anatafuta mwenza wa maisha.
Bado ninaamini jukwaa hili lina watu sahihi, na nina matumaini makubwa kuwa nitakutana na mtu mwenye malengo na nia kama yangu.
Kama wewe mwanamke unajiona una sifa hizo na uko tayari kwa hatua za maana, tafadhali niandikie DM na tuanze kufahamiana.
Asanteni sana kwa muda wenu na pia asante kwa kutenga nafasi ya kusoma andiko hili.