Natafuta nafasi ya kuichezea klabu yoyote inayoshiriki NBC Premier League Tanzania

Kwa huo umri unatakiwa uwe na kipaji kikubwa hasawa
Nenda mtibwa huwa mara nyingi km unauwezo hawakuwchi
 
Tumia vizuri mashindano ya ndondo cuo ukija Dar. Ila pia wakatiligi inapokwisha kusubiri msimu mungine timu nyingi sana zinaruhusu wachezaji kwenda kufanya majaribio.

Kwa umri ulionao wa miaka 26 ili utoboe unatakiwa uwe na kipaji extra ordinary ili uingie moja kwa moja kwenye nbc premier ligi. Yaani uwe na kipaji kuzidi kina ndemla, ambundo, kibu na wengineo.

Kila la kheri.
 
Ondoka huko nenda Dar, Kuna viwanja vingi vya majaribio kaanzie hapo. Kama una ndugu Dar muombe akupokee na kukuhost ukapambanie ndoto yako, Vipaji ni vingi sana mtaani, unahitaji sehemu ukaonekane si humu kwenye mtandao mdogo wangu.

Kila la heri.
 
Nimeshaanza mkuu, japo bado nina safari ndefu kidogo ya kuonekana.
 
Kwa miaka 26 na Bado ujatoka duh angalia mishe nyingine
 
Ondoka huko nenda Dar, Kuna viwanja vingi vya majaribio kaanzie hapo. Kama una ndugu Dar muombe akupokee na kukuhost ukapambanie ndoto yako, Vipaji ni vingi sana mtaani, unahitaji sehemu ukaonekane si humu kwenye mtandao mdogo wangu.

Kila la heri.
Ahsante sana dada yangu.

Wadau wengi wa JF hawanikubali ndugu yao (ndio maana timu zetu nyingi hazina mafanikio ndani na nje ya nchi maana wenye nia na juhudi hawakubaliki, ukilinganisha na wenye vipaji. Tumezoea kupondana, kupeana destructive feedback na hatuna roho ya kusaidiana kwa upendo). Halafu mtu akitoboa, ndio watu wanaanza kumkumbuka.

Ninao familia na ndugu huko Dar ila nawakwepa maana hawani'support kabisa japo wanajua kuhusu hiki kipaji changu. Watu wangu wengi wa karibu hawaniungi mkono pia mimi kuendeleza kipaji changu katika soka, Ila wanataka nitafute kazi na kuajiriwa (na kama unavyoona kwa sasa - hali ya ajira ni mbaya nchini).

Yaani ni bora hata ningekuomba wewe unipokee na uni'host kama upo Dar kwa kweli (ningekuwa tayari kusaidiwa na wewe).
 
Kwa miaka 26 na Bado ujatoka duh angalia mishe nyingine
Acha tu ndugu. Toka kipaji changu kionekane, nililazimika (na kulazimishwa) kugeukia masomo mpaka namaliza chuo.

Nimehangaika na kutafuta ajira, internship na volunteering bila mafanikio, lakini moyoni mwangu tangu nikiwa mdogo mojawapo ya passion yangu ni kucheza mpira. Usifikiri nilikuwa sifanyi kitu mpaka nafika umri huu! Ni vile tu bado sijabahatika.
 
Sasa mtu akikuomba video clip si umpe mshikaji akurekodi ?
Nenda hata wanakofanya mazoezi vijana jiunge nao mtu aku rekodi
Nilipokea mawazo yote ya wadau. Ila hivi vitu sio vya kukurupuka.
Nilikuwa kwanza natafuta sehemu wanakofanya mazoezi (na nimeshaanza).
Mpango upo na nimeshaanza kulifanyia kazi hilo.
 
Shukrani mkuu! Hiyo ni mojawapo ya ajenda zangu nikija Dar.

Hata kama kucheza Ligi kuu ya NBC itakuwa vigumu papo-hapo, sio vibaya nikaanza na daraja la pili halafu timu hiyo niliyoichezea ikapanda daraja na kuingia Ligi kuu msimu ujao. Au pia mbeleni naweza nikaonekana huko-huko na kuja kusajiliwa kwenye klabu inayoshiriki Ligi kuu.
 

Utafika tu, nenda taratibu,
 
Una miaka mingapi ?
Height yako ikoje ?
Uko mkoa gani ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…