Natafuta nafasi ya kuichezea klabu yoyote inayoshiriki NBC Premier League Tanzania

Natafuta nafasi ya kuichezea klabu yoyote inayoshiriki NBC Premier League Tanzania

Mpira haupo ivyo mkuu
Ni kweli, but that is according to bongo stigma.

Hii ni karne ya 21 na wote tumeshuhudia mambo mengi "impossible" yakiwa "possible", katika nyanja mbalimbali za maisha (Hata JPM na Colonel Sanders wa KFC walituonyesha mfano).

Katika mpira, hujawahi hata kusikia historia za kina Toni, Klose, Vardy na Drogba? Au unafikiri hayo hayawezekani kwa Tanzania? Kweli wakoloni walituharibu.

Soma kwanza hii post, ili ujifunze kitu.
15 Famous Soccer Players Who Started Playing Late
15 Famous Soccer Players Who Started Playing Late – Authority Soccer
 
Tafuta hata timu za daraja la tatu zinazoshiriki shirikisho
Katika kutafuta kwangu, bado sijapata kwa kweli. Ndio maana nimeona sio vibaya kuweka wazi uhitaji wangu huku, ili iwe rahisi kwa viongozi, makocha au wachezaji wa timu za daraja la 3 (au daraja lolote) kuniona hasa kama nao wanahitaji wachezaji kwa sasa (ni suala la wao kuniita tu kwenye kikosi).

Ila naendelea kufuatilia kwa wadau mbalimbali mtaani na mikoani kama naweza nikapata nafasi mahali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante sana dada yangu.

Wadau wengi wa JF hawanikubali ndugu yao (ndio maana timu zetu nyingi hazina mafanikio ndani na nje ya nchi maana wenye nia na juhudi hawakubaliki, ukilinganisha na wenye vipaji. Tumezoea kupondana, kupeana destructive feedback na hatuna roho ya kusaidiana kwa upendo). Halafu mtu akitoboa, ndio watu wanaanza kumkumbuka.

Ninao familia na ndugu huko Dar ila nawakwepa maana hawani'support kabisa japo wanajua kuhusu hiki kipaji changu. Watu wangu wengi wa karibu hawaniungi mkono pia mimi kuendeleza kipaji changu katika soka, Ila wanataka nitafute kazi na kuajiriwa (na kama unavyoona kwa sasa - hali ya ajira ni mbaya nchini).

Yaani ni bora hata ningekuomba wewe unipokee na uni'host kama upo Dar kwa kweli (ningekuwa tayari kusaidiwa na wewe).
Unfortunately mimi siishi Dar. Hapo ni changamoto kweli kweli.
 
Back
Top Bottom