Habari zenu wadau
Katika kutafuta maisha nmeamua kuanza ufugaji wa ngombe wa maziwa lakini sasa kupata pure breed anayetoa angalau 25 litres per day imekuwa changamoto.
Nimeshapigwa mara 2.
Naombeni mwenye connection na hawa ngombe aniunganishe
Unafugia wapi
na unataka ngombe wangapi
je Unajua ABC ya kufuga
Nikiwa kama mfugaji mstaafu nakushauri hivi
1. Anza na malisho,,,,,,narudia tena malisho....weka range ya miezi mitatu sita na mwaka,,,,inakuwaje unaweza kulima mahindi mtama..nakutengeneza silage, high yielding cow mkadirie KG 40 kwa siku
2. chanzo cha maji safi ya kunjwa kiwe cha uhakika
3. Banda, likinge mifugo yako na upepo, mvua na jua kali
4. Vijana angalau wajue abc za kumtunza ngombe,,,kumbuka ngombe 70% ni managament and 30% ni feeding
5. mbegu za ngombe sasa.....Jitahidi saana hapa usichemke kama upo maeneo ya JOTO usitafute pure breed..chotara inakufaa... hii itaadopt visuri..hapa inachukuliwa local cows kama borana na wengine wanapandikizwa mbegu pure cows
ukiweza pata fleckvieh cows hawa ni mazingira yote wanaishi ila upatiikanaji wake ni garama kidogo Kwa Tanganyika tupo wafugaji wachache saana wenye hii mbegu na majority hatuuzi
UTAPATAWAPI MBEGU.......usinunue kwa mtu ambaye hana taarifa za ngombe wake....nenda kwa mashamba makubwa mfano ASAS, Tanga fresh.....kwa ukand wa pwani kama upo huku Nenda MRUAzI TANGA wana mimbegu mizuri saana ya ngombe tena yenye mimba,,,ukipata connection ya mstaafu Kikwete.....utanishukuru baadae......kama upo nyanda za JUU watafute ASAS, Shamba la Philips, Kibebe nk wanambegu poa...Ukiwa kaskazini NENDA chuo cha mifugo tengeru au kituo cha serekali cha uhimilishaji utapewa connection ya watu na mashamba bora ya kununua Mifugo
kikubwa unaweza nunua hata NGOMBE MOJA TU ukamhudumia vizuri akakupa tija kuliko mwenye ngombe 05
la mwisho kila la kheri,,, ukifanikiwa usisahau kurudi hapa na glass ya Maziwa
Kidumu Chama cha Mapinduzi (((((joke))))