Exaud Minja
Senior Member
- Mar 13, 2009
- 100
- 13
Nawe pia toa wasifu kwasababu wapo wadada kibao wanatafuta wachumba pia ila hawajajitokeza kusema wazi, siunajua kina dada wanaona aibu kusema. Usisahau kusema kabila pia wengine wanaogopa makabila fulani fulani yanayojua kupiga mangumi na ambayo mama mkwe huwa anasauti kwenye nyumba zote za watoto wake wawe wa kike au wa kiume na ambayo mwanamke ni sawa na ng'ombe kuna kiboko maalumu cha kumchapia.
Nakushauri utafute mwenyewe, ila mwombe sana Mungu atakupatia unayehitaji watu wanaweza kusaidia kukuonyesha ila mambo mengine ukamaliza mwenyewe. Ujue makucha huwa yanafichwa kabisa kabla ya ndoa, ila mkishatoka kanisani tu yanakuwa huru kutokeza. Ila ukimpata uliyepewa na Mungu hayo yote hayatakuwepo.
Ukumbuke kupima afya yako na ya utakaye mpata kabla ya chochote na msubiri kupima tena miezi mitatu.
Ukumbuke kuwa tabia yako inaweza ikamharibu mwenzako au ikamgeuza mwenzako kabisa hata kama alikuwa changudoa akaacha kabisa akawa mama wa mfano wa kuigwa au kama alikuwa mtakatifu hata mwanaume hajamjua (Bikra) akawa malaya wa kutembea hata na ndugu yako wa damu.