Hongera sana mimi ni kijana ,mwenye future kubwa sana lakin sijaona kijana mwenye maono kama wew inshort umebalikiwa sana ,pia nina maoni kidogo japo unaruhusiwa kunikosoa
1: anza kwanza uzalishaji wa nguruwe then utajisajili badae ukisha fikisha target ya nguruwe uliyo panga,nafikir mwaka moja tuu.utakuwa umefikisha nguruwe si chini ya mia nane nikitoa hasara,
2: usiwaze kuhusu sokoo maana lipo la uhakika badala yake unaweza unaweza kuuza kwa bei ya jumla nguruwe mzima itaripaa sana ,
3 ungekuwa iringa ungefaidi zaid maana ,kutengeneza mabanda ungetumia mabanzi ,na kumimina tu chini maana huku mabanzi ni bure kabisa .
4 ukianza mradi wako tengeneza bustan za mbogaa itasaidia kuwalisha wanyama kam supriment ,vitamin na madim source,
5 jiepushe na kununua nguruwe piglet wa kizazi kimoja kuepushaa inbreeding huwa inasumbua kidogo,
Naamin utafanikiwa pia tupo nyuma yako kwa ajili ya mawazo na maoni mbalimbali pia soko tutakisaidiaa .
Sent from my X-TIGI_V11 using JamiiForums mobile app
Tembelea shamba hilo pengine wazo lako linaweza kupata mahala pakuanzia.
Hao jamaa kwa sasa zoezi lakuongeza thamani nyama kwa taarifa iliyopo imewashinda/wameacha .Kajifunze hapo kwanini walikwama.
Kitengo cha pumba haswa za mpunga nipo hapa...Habari wadau.
Mimi ni Mtanzania niliyebahatika kupata elimu katika nchi mbalimbali za Bara la Ulaya. Baada ya kumaliza elimu yangu nimerejea nchini kujenga taifa.
Kufuatia changamoto ya ajira nimeonelea nichukua route ya kujiajiri. Baada ya kufanya utafiti wa kina, nimejiridhisha kuwa mradi wa Ufugaji wa Nguruwe kibiashara (Commercial Piggery Project) unaweza lipa katika muda mfupi.
Lengo langu sio tu kufuga Nguruwe, bali kufuga na kuongezea thamani bidhaa nitakazizozalisha ili kuuza bidhaa hizo Kwenye upper-end market.
Nafahamu wapo watanzania wenye mitaji ila hawana muda wa kufanya mradi wa aina hii. Mimi nina ardhi kubwa kando ya mto Ruvu, access ya kupata soko zuri na elimu ya kutosha ambayo ninatarajia kuitumia katika mradi huo.
Hivyo nakaribisha wenye mitaji ya hali (Relevant education) na Mali (Fedha) ktk kufanikisha mradi huu.
Mambo yote yataenda kisomi/kisheria.
Karibuni sana
Kaka kwema, tunaweza kuwasiliana Whatsapp tujue kama tunaweza kufanya mradi huu?
Hujawa specific kwenye kiasi cha pesa kama mtaji unaotakiwa. Kama unajua unachoenda kukifanya basi utakuwa unajua mtaji unaotakiwa
Kitengo cha pumba haswa za mpunga nipo hapa...
Poa usijar ndugu pamoja sna[emoji122][emoji122][emoji122]Ahsante Sana Kwa ushauri na link.
Naomba nitoe maoni yangu japo naweza kuwa na uandishi mbaya, ila ujitahidi kunielewa. Hii miradi ya ufugaji wa nguruwe mimi nilishawahi kufanya. Kwa kifupi zipo changamoto tena kubwa.
1. Ufugaji wowote ambao utanunua nguruwe then ukawapandisha na kuzalisha wototo, ufugaji huu ni hatari na utakupelekea kwenye hasara. Maana mara nyingi vifaranga wanakufa na wanaugua mara kwa mara. Pia ukuaji wao una shida, hivyo kuwa na vifaranga ambao sio wazuri. Waliodumaa
Nini ufanye? Nunua vifaranga wa nguruwe wa miezi mitatu (wapo wengi tu huku mitaani) ambao ni wazuri na wakubwa kiasi. wewe unaenda kuwalisha na ukishaona wamefikia ukubwa ambao wewe unaona wanafaa kwa biashara. Fanya biashara.
2. Soko la nguruwe lipo japo sio zuri kama unavyofikiri. Mara nyingi tunauza nguruwe wa wastani wa kilo 80-100 kwa kati ya shilingi 300000-350000/=. Na kuna kipindi Tunakosa wateja. Kiasi kwamba nguruwe aliyestahili kuuzwa unaendelea kumlisha kwa wiki kadhaa. Hii ni kutengeneza hasara. Hivyo soko huwa linapanda na kushuka kulingana na uhitaji. Kumbuka nguruwe wanafugwa karibu kila pembe ya hii nchi.
3. Kwa ufugaji wako wa kisomi (mimi sijasoma) naona unakwenda kushindwa kabla ya kuanza. Kivipi? Mara nyingi sisi tusiosoma na hatuna tabia ya kuweka kumbukumbu ya gharama tulizotumia kuanzia kununua vifaranga, vyakula, madawa, na kulipa mfanyakazi, tungekuwa tunaorodhesha vyote hivyo walllah tusingeweza kuuza kwa hizo bei za 300-350k. Tungeona hasara. Maana kifaranga mzuri tunanunua kwa shs 70-80k ndio uanze kumtunza.
Na si kweli kwamba kifaranga wa miezi mitatu ukimnunua unamlisha au kumtunza kwa miezi 6 kama ulivyosema. Utamtunza kwa zaidi ya mwaka. Vyakula na madawa + mfanyakazi + muda hata ukimuuza kwa 400k halipi.
Sasa kwa usomi wako jiandae kuorodhesha kila gharama afu uje uuze kwa bei unazosema uone kama utapata mteja. Nakuhakikishia hapa hasara ipo wazi.
Ushauri wangu kwako. Tafuta mtaji, jenga banda la kutosha nguruwe 50-80 wakubwa. Nenda mikoani nunua nguruwe wazuri kwa bei ya ukandamizaji. Safirisha mpaka hapo ruvu. Washushe. Chinja na Anza kuwaongezea thamani kama ulivyosema. Lakini hili wazo la kuwafunga, uwakuze mpaka wakue utapitia changamoto nyingi na nyingine ngumu.
Kazi njema
Nimeipenda hiyo plan na pia napenda sana nikiona kijana wa ndani ya bongo kaja na plani nzuri ya biashara. Shida yangu ni moja tu huwa sipendi biashara ya watu wa 2 napenda iwe group ya watu au only mwenyewe, kama utaweza pata watu wengine na kuanza as group ya watu ianzishwe kampuni na kila mtu anunue shea niko tayari kuweka 15 to 20 M hata leo . Tupeane update tu.
Ok.Ahsante kiongozi. Nashkuru Kwa utayari wako. Nitakupa updates.
Tatizo la vifaranga kufaa la sababishwa na muingiliano wa vizazi{inbreeding} hivo akiwa makin atakuwa sawaa.
Hongera ndugu kwa mawazo mazuri ya kijasiriamali!
Una malengo makubwa na mazuri. Sisi ni wazoefu wa miaka mingi katika ufugaji.Inafaa kuanza kidogo kwa malengo makubwa(Start Small Dream big).
Waweza tufuata kwenye page yetu ya instagram;nna imani kuna mengi utajifunza katika ndoto yako: