Natafuta Serious Partner wa Kuanzisha Mradi Mkubwa Wa Nguruwe Tanzania

Natafuta Serious Partner wa Kuanzisha Mradi Mkubwa Wa Nguruwe Tanzania

Ahsante Sana kiongozi Kwa busara na maoni yako. Kwa utafiti nilioufanya. Nimejiridhisha kuwa soko kubwa na la uhakika lipo Dar Es Salaam na Zanzibar. Hivyo kufugia mbali na maeneo haya ni kujiongezea gharama za uzalishaji hasa Kwa kusafirisha Nguruwe hai. Hivyo ni bora ulete mabanzi toka Iringa na chakula mana havina urasimu Kwenye kusafirisha kuliko kusafirisha Nguruwe hai uliyemfugia Mkoani.
Hongera sana mimi ni kijana ,mwenye future kubwa sana lakin sijaona kijana mwenye maono kama wew inshort umebalikiwa sana ,pia nina maoni kidogo japo unaruhusiwa kunikosoa
1: anza kwanza uzalishaji wa nguruwe then utajisajili badae ukisha fikisha target ya nguruwe uliyo panga,nafikir mwaka moja tuu.utakuwa umefikisha nguruwe si chini ya mia nane nikitoa hasara,
2: usiwaze kuhusu sokoo maana lipo la uhakika badala yake unaweza unaweza kuuza kwa bei ya jumla nguruwe mzima itaripaa sana ,
3 ungekuwa iringa ungefaidi zaid maana ,kutengeneza mabanda ungetumia mabanzi ,na kumimina tu chini maana huku mabanzi ni bure kabisa .
4 ukianza mradi wako tengeneza bustan za mbogaa itasaidia kuwalisha wanyama kam supriment ,vitamin na madim source,
5 jiepushe na kununua nguruwe piglet wa kizazi kimoja kuepushaa inbreeding huwa inasumbua kidogo,
Naamin utafanikiwa pia tupo nyuma yako kwa ajili ya mawazo na maoni mbalimbali pia soko tutakisaidiaa .

Sent from my X-TIGI_V11 using JamiiForums mobile app
 
Ahsante Sana Kwa ushauri na link.
Tembelea shamba hilo pengine wazo lako linaweza kupata mahala pakuanzia.
Hao jamaa kwa sasa zoezi lakuongeza thamani nyama kwa taarifa iliyopo imewashinda/wameacha .Kajifunze hapo kwanini walikwama.

Habari wadau.

Mimi ni Mtanzania niliyebahatika kupata elimu katika nchi mbalimbali za Bara la Ulaya. Baada ya kumaliza elimu yangu nimerejea nchini kujenga taifa.

Kufuatia changamoto ya ajira nimeonelea nichukua route ya kujiajiri. Baada ya kufanya utafiti wa kina, nimejiridhisha kuwa mradi wa Ufugaji wa Nguruwe kibiashara (Commercial Piggery Project) unaweza lipa katika muda mfupi.

Lengo langu sio tu kufuga Nguruwe, bali kufuga na kuongezea thamani bidhaa nitakazizozalisha ili kuuza bidhaa hizo Kwenye upper-end market.

Nafahamu wapo watanzania wenye mitaji ila hawana muda wa kufanya mradi wa aina hii. Mimi nina ardhi kubwa kando ya mto Ruvu, access ya kupata soko zuri na elimu ya kutosha ambayo ninatarajia kuitumia katika mradi huo.

Hivyo nakaribisha wenye mitaji ya hali (Relevant education) na Mali (Fedha) ktk kufanikisha mradi huu.

Mambo yote yataenda kisomi/kisheria.

Karibuni sana
Kitengo cha pumba haswa za mpunga nipo hapa...
 
Hujawa specific kwenye kiasi cha pesa kama mtaji unaotakiwa. Kama unajua unachoenda kukifanya basi utakuwa unajua mtaji unaotakiwa
 
Kwa mtazamo wangu majadiliano ya kiasi cha mtaji kinapaswa kujadiliwa na interested parties. Kama nilivyoeleza mtaji una vary kutegemeana na mnachotaka kufanya. Hivyo tukishaafikiana, wale watakaopenda tutakutana na kujadiliana suala Hilo Kwa kina. Hapa nimewasilisha mada tu. Hizo details itapendeza zikijadiliwa na wanahisa/interested partners.
Hujawa specific kwenye kiasi cha pesa kama mtaji unaotakiwa. Kama unajua unachoenda kukifanya basi utakuwa unajua mtaji unaotakiwa
 
Naomba nitoe maoni yangu japo naweza kuwa na uandishi mbaya, ila ujitahidi kunielewa. Hii miradi ya ufugaji wa nguruwe mimi nilishawahi kufanya. Kwa kifupi zipo changamoto tena kubwa.

1. Ufugaji wowote ambao utanunua nguruwe then ukawapandisha na kuzalisha wototo, ufugaji huu ni hatari na utakupelekea kwenye hasara. Maana mara nyingi vifaranga wanakufa na wanaugua mara kwa mara. Pia ukuaji wao una shida, hivyo kuwa na vifaranga ambao sio wazuri. Waliodumaa

Nini ufanye? Nunua vifaranga wa nguruwe wa miezi mitatu (wapo wengi tu huku mitaani) ambao ni wazuri na wakubwa kiasi. wewe unaenda kuwalisha na ukishaona wamefikia ukubwa ambao wewe unaona wanafaa kwa biashara. Fanya biashara.

2. Soko la nguruwe lipo japo sio zuri kama unavyofikiri. Mara nyingi tunauza nguruwe wa wastani wa kilo 80-100 kwa kati ya shilingi 300000-350000/=. Na kuna kipindi Tunakosa wateja. Kiasi kwamba nguruwe aliyestahili kuuzwa unaendelea kumlisha kwa wiki kadhaa. Hii ni kutengeneza hasara. Hivyo soko huwa linapanda na kushuka kulingana na uhitaji. Kumbuka nguruwe wanafugwa karibu kila pembe ya hii nchi.

3. Kwa ufugaji wako wa kisomi (mimi sijasoma) naona unakwenda kushindwa kabla ya kuanza. Kivipi? Mara nyingi sisi tusiosoma na hatuna tabia ya kuweka kumbukumbu ya gharama tulizotumia kuanzia kununua vifaranga, vyakula, madawa, na kulipa mfanyakazi, tungekuwa tunaorodhesha vyote hivyo walllah tusingeweza kuuza kwa hizo bei za 300-350k. Tungeona hasara. Maana kifaranga mzuri tunanunua kwa shs 70-80k ndio uanze kumtunza.

Na si kweli kwamba kifaranga wa miezi mitatu ukimnunua unamlisha au kumtunza kwa miezi 6 kama ulivyosema. Utamtunza kwa zaidi ya mwaka. Vyakula na madawa + mfanyakazi + muda hata ukimuuza kwa 400k halipi.
Sasa kwa usomi wako jiandae kuorodhesha kila gharama afu uje uuze kwa bei unazosema uone kama utapata mteja. Nakuhakikishia hapa hasara ipo wazi.

Ushauri wangu kwako. Tafuta mtaji, jenga banda la kutosha nguruwe 50-80 wakubwa. Nenda mikoani nunua nguruwe wazuri kwa bei ya ukandamizaji. Safirisha mpaka hapo ruvu. Washushe. Chinja na Anza kuwaongezea thamani kama ulivyosema. Lakini hili wazo la kuwafunga, uwakuze mpaka wakue utapitia changamoto nyingi na nyingine ngumu.

Kazi njema
 
Ahsante Kwa ushauri wako.

Nimeipenda hiyo plan na pia napenda sana nikiona kijana wa ndani ya bongo kaja na plani nzuri ya biashara. Shida yangu ni moja tu huwa sipendi biashara ya watu wa 2 napenda iwe group ya watu au only mwenyewe, kama utaweza pata watu wengine na kuanza as group ya watu ianzishwe kampuni na kila mtu anunue shea niko tayari kuweka 15 to 20 M hata leo . Tupeane update tu.
 
Ahsante kiongozi. Nashkuru Kwa utayari wako. Nitakupa updates.
Nimeipenda hiyo plan na pia napenda sana nikiona kijana wa ndani ya bongo kaja na plani nzuri ya biashara. Shida yangu ni moja tu huwa sipendi biashara ya watu wa 2 napenda iwe group ya watu au only mwenyewe, kama utaweza pata watu wengine na kuanza as group ya watu ianzishwe kampuni na kila mtu anunue shea niko tayari kuweka 15 to 20 M hata leo . Tupeane update tu.
 
Tatizo la vifaranga kufaa la sababishwa na muingiliano wa vizazi{inbreeding} hivo akiwa makin atakuwa sawaa.
 
Hongera ndugu kwa mawazo mazuri ya kijasiriamali!
Una malengo makubwa na mazuri. Sisi ni wazoefu wa miaka mingi katika ufugaji.Inafaa kuanza kidogo kwa malengo makubwa(Start Small Dream big).
Waweza tufuata kwenye page yetu ya instagram;nna imani kuna mengi utajifunza katika ndoto yako:
 
Tatizo la vifaranga kufaa la sababishwa na muingiliano wa vizazi{inbreeding} hivo akiwa makin atakuwa sawaa.

Mbali na masuala ya inbreeding. Ni vyema tukafahamu kuwa matunzo atakayoyapata Nguruwe anayezaliwa masaa machache baada ya kuzaliwa, yatadefine Nguruwe huyu atakuwaje maishani mwake.

Watoto wa Nguruwe chini ya week 2 wanakuwa na passive immunity badala ya active immunity. Kimsingi kinga dhidi ya magonjwa huipata kutoka Kwa mama Yao kupitia maziwa. Hivyo, tatizo linaanziaga toka Kwenye afya ya Nguruwe mama. Kama mama hakulishwa vzr wkt wa ujauzito, hatoweza toa maziwa yenye virutubisho vya kutosha vitavyoweza mjengea mtoto kinga ya kutosha kupambana na magonjwa mara baada ya kuzaliwa.

Zaidi ya kumlisha vzr Nguruwe wkt wa mimba, mfugaji anapaswa kuheshimu ratiba ya chanjo ya Nguruwe wake. Kwa mfano mama mjamzito anapaswa achomwe chanjo ya kuzuia watoto watakaozaliwa ili wasiharishe week mbili kabla maana chanjo hukua muda wa Hadi siku 10 kufika Kwenye maziwa. Sasa mfugaji usipo heshimu ratiba ya chanjo, unaweza mpa chajo hiyo siku mbili kabla hajazaa, so by the time Nguruwe anazaa unakuta chanjo uliyomchoma mama haijafika Kwenye maziwa hivyo watoto wanazaliwa na kunyonya maziwa yasiyo na hiyo chanjo. Na Hivyo watoto hukosa passive immunity toka Kwa mama zao.

Pia mfugaji unapaswa kuhakikisha watoto wanaozaliwa wananyonya maziwa ya awali (ndani ya masaa 24 ya mwanzo) (Colostrum) mana kupitia haya maziwa ya awali ndio Nguruwe hupata nguvu na kinga dhidi ya magonjwa yanayowanyemelea mara baada ya kuzaliwa. Hivyo mfugaji anapaswa kuhakikisha anasaidia watoto kunyonya mara baada ya kuzaliwa.

Aidha, mfugaji anapaswa kuhakikisha anasaidia kukausha vitoto baada ya kuzaliwa na anawapa joto kwani joto la nje sio Sawa na la ndani ya tumbo. Hivyo usipovikausha na kuvipa joto la kutosha, vitoto vitatumia nguvu nyingi kuzalisha joto (Kwa kutetemeka) badala ya kutumia nguvu hiyo kunyonya.

Ukiangalia Kwa umakini haya niliyoyaeleza utagundua kuwa uhai wa makinda ya Nguruwe haupaswi kuwa ni suala la bahati nasibu. Yapo mambo ukiyafanya yatakupa matokeo chanya. Ukweli ni kwamba wafugaji wengi wa kitanzania hasa wanaotegemea Shamba boy hawafanyi haya. Hivyo namna pekee ya kuondokana na vifo vya utotoni ni kuongeza umakini katika kusimamia Nguruwe wako. Wapo wafugaji wengi ambao ni wazoefu ila hawaheshimu haya niliyoyaeleza. Hivyo mfugaji mpya unatakiwa ujifunze toka kwa mzoefu anayefahamu nini anafanya, vinginevyo, utakuwa discouraged bila sababu. Kumbuka kinachotofautisha mfugaji/mfanyabiashara anayepata faida na yule anayepata hasara (katika biashara hiyo hiyo) ni namna wanavyofanya ufugaji/biashara yao.
 
Ahsante sana MalafyaleP. Nitatembelea site yako.
Hongera ndugu kwa mawazo mazuri ya kijasiriamali!
Una malengo makubwa na mazuri. Sisi ni wazoefu wa miaka mingi katika ufugaji.Inafaa kuanza kidogo kwa malengo makubwa(Start Small Dream big).
Waweza tufuata kwenye page yetu ya instagram;nna imani kuna mengi utajifunza katika ndoto yako:
 
Kwa makadirio tu itahitajika 100,000,000+ kwa, hali ya mifuko ya wengi + uaminifu na watanzania tulivyo wataalam kwenye risk cakculation utaambulia kuungwa mkono kwa kauli tu badala ya vitendo.

Nashauri upange mradi wako ktk hatua/phases hata 4. kama unaanza na banda la banzi+nguruwe 10 utakaowauza hai itapendeza.

Baada ya kuona faida panua banda, ongeza mbegu mara mbili au tatu

Hatua ya 3 jenga miundombinu kwa kutumia faida na kuanza kusaka wadhamini+wadau wa kuunga juhudi tyr ukiwa na kianzio.

Mwisho panua soko lako ulilolenga (hotels), vyombo na mabanda ya kisasa sanjari na usajili ktk mamlaka husika ukiwa umeshaonja matunda.

Nchi yangu ya Tanzania imejaaliwa watu wenye vipawa vyote, wajuaji, wakatisha tamaa, werevu wa kusigana, matapeli wa kila hali, washirikina na non risk takers (sijui niisemeje kwa kiswahili) . usitegemee atokee mtanzania akuamini kwa maneno matupu tu hayo na hesabu zako za kisomi (iweke sawa hesabu za makaratasi) badala yako watakuwela kundi moja na wale inspiration speakers; wanahamasisha kilimo cha biashara mf. bustani kuwa unatumua milioni 1 ulivuna unapiga milioni 10. amini bure ekari 3 bila hatua uliyokwishapiga kuelekea wazo lako, hazitoshi kumshawishi mtu amwage pesa.

Nimi ni miongoni mwa watanzania wagumu kumuamini msomi wa nchi hii kwa taaluma ya uchumi. maramia nimwamini mwanasiasa na ahadi zake maana huwa nimejindaa kisaikolojia kwa kitakachofuata, huwa wanaanguka lakini baada ya kujaribu na hakika hututia matumaini kuwa awamu ijayo watafanikisha. laiti maafisa ugani na bw/bi. kilimo wangekuwa lau na mashamba darasa ya lau rbo heka kutuwekea elimu zao kutoka makaratasi kuwa vitendo ingefaa kunibadili.

Naungana na mchangiaji hapo juu.

Sisi ambao hatukusoma/hatukubahatika kuajiriwa hakuna fursa ambazo hatujajaribu. kilimi, ufugaji, biashara, viwanda vidogo (vyerehani, mashine za, mbao na nafaka) we speak frankly from experience. ni msomi tu anatuchukulia poa kwa vile anatuzidi hesabu

Hitimisho :
Unda kundi la jamaa zako pengine school mates,members wa grp za whatsap, work mates mchangishane hata 500,000 au m1 kwa watu kama 10/20 mjenge credibility, hapo tutawapokea kirahisi hata kwa kutuuzia hisa (chonde tu zisije kuwa km za voda).

KILA LA KHERI!
 
Back
Top Bottom