Natafuta tiba ya tonsils sugu bila kufanyiwa operation

Natafuta tiba ya tonsils sugu bila kufanyiwa operation

Mfano kituo gani cha afya kwa dsm?

Nenda hospital za serikali kuna madaktari bingwa wa koo, pua na masikio (ENT surgeons) naamini huko gharama ya operation hiyo itakuwa chini ya million 1

Kila la kheri.
 
Hii acha niisome labda nitaokota kitu. Kiufupi nina dada yangu anasumbuliwa sana na hizo tonsilz. Mwaka 2017 alifanyiwa op ya kuziondoa pale regency tukaona jambo limekwisha. Ajabu tangu mwaka wa jana 2025 march ,tonsils zimemrudia tena kwa speed ya sgr, zinamtesa sana na op h anaona kama haikumsaidia maana aliamini baada ya op changamoto itakua imemalizika 100%
 
Na mimi kuna auntie yangu zilirudi baadae after operation.
Tuendelee kuomba Mungu, ndio maana nikipata mtu wa tiba za asili nitafurahi sana.
 
Tonsillitis ni ugonjwa unanisumbua karibu miaka 7 sasa ila currently zimefikia hatua mbaya.

Nikimeza dawa siponi na nikichoma sindano zinapoa kisha zinarudi tena.

Siwezi maliza mwezi au miezi miwili sijalala kitandani sababu ya tonsils.

Nishajaribu dawa za kienyeji za kukoroga mchanganyo.

Antibiotics napiga zile kali kali kama koact na sindano sometimes.

Nilishawai enda kwa Ekenywa nikaonana na Dr akanicheki kwa screen akasema nipo level ya kufanya surgery yatolewe.

Kwa sasa sina bima ya afya na sina hela ya kutosha maana aliniambia OP yake ni kama million.

Pia kwa nature ya kibarua changu ata nikipitisha bakuli nikafanye operation, kazi haiwezi nisubiri mwezi mzima wa kujiuguza nitakuta washani replace.

So bado sijakata tamaa ya kupona.

Noamba mwenye uzoefu wa tiba mbadala halisia sio feki anisaidie mawazo, au hata tiba ya hospital ambayo inawezekana sijawai ifanya anasaidia mawazo. huu ugonjwa kuna muda nahisi unaweza niua maana umeniganda sana.

Karibuni mnisaidie!
Kila siku tunawaambia mkiumwa nendeni hospitali mkatibiwe acheni kuleta ujuaji kwenda pharmacy kujinunulia dawa kiholela matokeo yake mnapewa zile dawa kali zaidi kiasi kwamba zikifeli mnakosa mbadala.

Hapo cha msingi kaonane na daktari wa koo umuelezee tatizo lako
 
Haya sawa nimekuelewa mkuu.
 
Back
Top Bottom